Nimeishi uchagani (Rombo) maisha yangu yote, na hiyo ulotaja ni salamu za kichaga kwa mtu aitwaye Clement. Wachaga, kama binadamu wengi walivyo, wanapenda sana kufupisha majina ya watu.Kwa hiyo Joseph itafupishwa na kuwa Josee, Rodrick itakuwa Rodii, Godfrey au Godbless yanakuwa Godii,Grace itakuwa Gree, Joyce itakuwa Joii, Mary inakuwa Merii, Matilda=Mati nk. Katika sredi hii mhusika ni Clement ndo maana anasalimiwa kama Clemeee! Majina ya ukoo ni nadra sana kufupishwa;yanatamkwa full eg Moshi=Moshi.Swai=SWai Massawe=Massawe etc.Bahati mbaya uchagani hakuna majina marefu ya ukoo kama ilivyo uhayani Ndo maana hakuna ufupisho kwenye majina ya ukoo.
Akina mama uchagani ndo mafundi wakubwa wa kufupisha majina ya watu.
Kwa hiyo kama ni Matilda anasalimiwa, utasikia:Shimbony shafo Matii! nk.