WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 949
Je, umewahi kusikia kuwa wachaga pindi wapendwa wao wanapofariki basi baada ya muda fulani kupita huenda kufukua mabaki ya miili ya maiti wao kisha kuwahifadhi sehemu maalumu?Kwanza kabsa nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na makabila tofauti tofauti ambayo yametofautiana katika mila na desturi, hivyo mila ya kabila moja huweza kuwa ni kitu cha kushangaza sana kwa kabila lingine. Leo nimekuletea jambo la tofauti kidogo linalowahusu wachaga.
Tuanzie hapa wachaga wana mila ya kutofikisha msiba usiku yaan kwa mfano mtu kafariki dar atasafirishwa kwenda kilimanjaro ila ikiwa safari itakuwa ni ya usiku basi kabla ya kuingia kijiji au mahali msiba utakapozikwa basi watalala kijiji cha jirani ili msiba ukafike kesho asubuhi.
Wao kwao ni nadra sana msiba kufikisha usiku Inasemakana sababu zinazopelekea kufanya hivyo kwanza ni kuepusha kuzua taharuki kwa wafiwa na majirani kuanza kuomboleza mapema, na kupiga kelele haipendezi. Pili ni imani na mila kuwa mwili wa marehemu ukifika unatakiwa kwenda kuzikwa Moja kwa moja.
KUFUFUA WAFU
Vilevile jambo lingine linaloweza kuwa geni kwa makabila mengine lakini ni utamaduni wa wachaga hasa wa kilema mkoani kilimanjaro ni hili la kuwafufua wapendwa waliofariki kila inapotimia miaka 8 au 10 baada ya kuzikwa. Mila hiyo ina taratibu Zake za kufuata kabla ya kufikia hatua ya mwili kufukuliwa sehemu iliyokuwa umezikwa na kwenda kuwahifadh sehemu nyingine, kitendo hiki kimekuwa kikifuata utaratbu maalumu wa kimila na kisipofanywa inaaminika kuwa na madhara makubwa kwa ukoo hasa kusababisha kifo.
Hivyo baada ya Maiti kufikisha miaka 8 au 10 wanafamilia huandaa vitu vinavyohitaji kisha humuita mtaalamu au mtu mila awasaidie kwenye masuala ya kufukua kwani sio kila mtu anaweza kuifanya hiyo kazi.
UTARATIBU WA KUFUKUA
Siku moja, kabla ya saa kumi alasiri mzee wa mila ataotesha jani la Sale pamoja na kumwaga pombe ya mbege juu ya kaburi ambalo mtu anatakiwa kufufuliwa. Kesho yake asubuhi mzee wa mila huenda kuangalia kama jani hilo limenyauka au laah!!, kama halijanyauka ni ishara ya kwamba ya kwamba wakifukua kaburi hilo watakuta mafuvu ya mhusika, basi hapo Huchinjwa mbuzi na kunena maneno yanayotakiwa kuzungumzwa wakati anamwaga damu katika kaburi.
Kisha wanaukooo wanaanza kufukua kaburi huku akiwaelekeza vitu vya kufanya, shughuli ya kufukua huendelea huku akina mama wakiendelea na shamrashamra za kupika maana inakuwa ni sherehe Kubwa. Mara tu watakapoanza kuona mabaki ya marehemu basi watasitisha kila kitu hapo wanawake wataruhusiwa kusogolea eneo hilo na kupiga vigeregere, kisha huwpa chakula wanaukoo.
Kwakuwa kazi huchukua muda mrefu basi inabidi kula na kunywa. Baada ya vigeregere kumalizika fuvu la Mhusika huchukuliwa kuwekwa kwenye jani la sale kisha kuhifadhiwa ndani. Fuvu hilo likishahifadhiwa ndani ni ishara ya kuwa mtu huyo ni hai na ci mfu tena kwa imani za wachaga wa kilema. Kesho yake asubuh na mapema hulichukua fuvu hilo na kulipaka mafuta ya "msuka samli" na kisha Kulifanyia mila zingine. Mzee wa mila atalishika fuvu hilo kisha wanaukoo huja mmoja mmoja kulipaka mafuta fuvu hilo huku kila mmoja akiomba anachokihitaji.
Baadaye ataungana na wanaukoo kwa idadi sawa ya jinsi na wataelekea sehemu ya kulihifadhi "mbuoni". Wakati wanaelekea.
Mbuoni, Masharti ni kuwa hawaruhusiwi kugeuka nyuma, hadi wanapofika sehemu wanapoweka fuvu hilo.
Inasemakana pia baadhi ya sababu kufanya hivyo ni kutokana na ufinyu wa ardhi hali inayosababisha kuendeleza mila hiyo tangu enzi za mababu na mababu.