Wachambuzi Maarufu wa Soka na uchaguzi TFF

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wanabodi,

Ally Mayai nimemfahamu miaka mingi akiwa mchezaji hadi sasa. Ingawa sijawahi kuwa na ukaribu nae lakini kwa kufatilia uchambuzi wake wa soka, umakini wake na hekima ambayo pia alikuwa akisifiwa toka akiwa mchezaji vinanipa msukumo wa kuamini anafaa kuwa kiongozi TFF. Baadae kupitia mdahalo TBC pengine nitapata fursa ya kuona potential za wagombea wengine.

Nimeona comments za baadhi ya wachambuzi wenzake kutomuunga mkono Ally Mayai ingawa hawasemi wazi. Pia nilitegemea hao wachambuzi kuwa mstari wa mbele kumpigia debe mwenzao lakini ni kama wamempotezea hivi. Kama kawaida yao wanataka baada ya uchaguzi ndio waanze kukosoa. Ukiwasikia wakichambua michezo hasa soka na jinsi wanavyoponda soka letu nilitegemea kuwasikia sana kipindi hiki cha uchaguzi tena hasa mwenzao alipojitokeza kuwawakilisha ili warekebishe kile wanachopigia kelele kila siku.
Kwakuwa mmeamua kuwa kimya ikiwemo kutosaidia kumnadi mwenzenu au walau kusema mgombea yupi mnaamini ni sahihi....tusiwasikie baada ya uchaguzi na chambuzi zenu za kuponda viongozi ....huu ndio wakati sahihi wa kushauri ili tupate viongozi bora.

Mpaka sasa sijaona makala makini kuchambua wagombea na uwezo wao ili kusaidia wajumbe wapate wasifu kwa undani kabla ya uchaguzi. Fursa ni hii tukipata garasa tusianze kuja na makala za kujifanya tulijua kitachotokea.
 
Sasa subiri mjue unafiki wetu ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…