Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 24,314
- 38,919
Habari wana sports,
Niendelee moja kwa moja kwenye hoja yangu, tangu Yanga yangu ilipokuwa inasuasua mtu aliyerushiwa maneno ni Kocha mkuu Mwinyi Zahera kwamba hana mbinu sahihi, anawachezesha baadhi ya wachezaji out of position, anashindwa kuiunganisha timu, Mara yupo juu ya Yanga hakuna anayeweza kumwambia kitu kwasababu anaisaidia Yanga kwaPesa zake mfukoni na maneno mengiiiiii ya kejeli.Hao hao waandishi za michezo na kelele zao baada ya Mwingi kwenda rikizo na timu ukiwa pre season, walipiga sana kelele, leo ndiyo wa kwanza kumuarika kwenye redio zao na wao kujifanya kumuonea huruma.
Hayo yote yalisemwa na hawa wanaojiita waandishi na wachambuzi nguli wa soka Tz.Kiwango cha Tanzania kuwa hapa hata hawa nao wanachangia maana wanaongea maneno mengi bila takwimu,nikama wanasiasa tu na baadhi ya waandishi wanatumia mic kishabiki sana.
Nikweli Zahera ameisaidia Yanga na alivumilia katika kipindi kigumu sana, na aliendesha harambee kadhaa ambazo kwa wale tulikuwa tunaenda viwanjani msimu uliopita ulienda na pesa ya kiingilio pale taifa unabeba na hela ya kapu lililokuwa linapita kiwanjani ilikusupport team. Mimi ni mmoja wapo wa mtu aliyekuwa anamkubali sana mwingi, ila Kwasasa niseme ukweli nilikuwa sitamani hata kumuona na kufukuzwa kwake nifuraha kubwa sana
Zahera alipoteza weledi kama mwalimu wa mpira, alikuwa amelewa sifa na kusahau kazi yake iliyomleta nchini.heshima aliyopewa alijiona hakuna wakumwambia kitu klabuni.
Kila baada ya mchezo Mwinyi hakosi sababu, na mara nyingi huwa hatoi sababu za kiufundi anapiga blabla tu, juzi anatoka Egypt anasema yaani "Vijana walipambana sana hadi kocha wa Pyramids alikuwa anashangaa", sasa kocha kapigwa 3-0 anajisifu. Kabla ya mchezo wa Pyramids Kirumba "lazima tupate ushindi nyumbani ili tuwe kwenye nafasi nzuri ya kufuzu", baada ya game " hatukujiandaa kucheza mashindano haya na hatuna wachezaji wa kupambana na Pyramids ". Ana kauli nyingi za utata na za kuonyesha kutokuwa na weledi kabisa, japo na viongozi wa hizi timu zetu za urithi wa na changamoto zao ila kwa Mwinyi walikuwa hawana namna zaidi ya kutimua.
Pamoja na mazuri ulioitendea Yanga ila hakuna budi kusema kwaheri viongozi wamefanya maamuzi sahihi, kama unatudai utalipwa tu,Yanga ipo itaendelea kuwepo na tutaiacha.
Daima mbele, Nyuma mwiko