Ongelea kuhusu umuhimu wa timu ya taifa na nini kinafaa ili kusaidia ushindi wa timu ya taifa. Kama Bongozozo mzungu anacho cha kusema kuhusu timu ya taifa wewe mwandishi wa habari mwenye kipaza sauti unashindwa nini kupata cha kuongelea?. Kuna vitu mimi vilinifanya mimi niachage kuhangaika na timu ya taifa ambavyo ni pamoja na:
1. Raia namba moja kuikatia tamaa timu yake ya taifa hadi akaiita kichwa cha mwenda wazimu. Kama yeye kasema hivyo mimi ni nani?
2. Uteuzi wa timu ya Taifa. Kuna tatizo la kuangalia wangapi wametoka Simba na wangapi watatoka Yanga bila kuzingatia mahitaji ya timu.
3. Viongozi na wanasiasa kujitokeza siku moja kabla ya mechi na ahadi kedekede. Wanataka ng'ombe anenepe siku ya mnada tu.
4. Jezi ya timu ya taifa. Jezi ya timu ya taifa lazima iwe kali sana/quality ya kutosha kutoka makampuni yanayoeleweka na serikali ina subsidize bei ya jezi hiyo ili kila mtu aipate ikiwa na ubora uleule . Sio matambara yenye nembo ya mdhamini ya timu fulani.
5. TFF/Serikali washirikishe watanzania kwenye timu yao kwa njia mbalimbali kama vile kucheza bahati na simu kwa washindi kusafiri na timu yao na zawadi nyingine za papo kwa papo uwanjani kwa waliohuduria ikiwa ni pamoja na burudani mbalimbali uwanjani siku ya mechi.