Wachambuzi pia huchambuliwa

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
7,621
Reaction score
12,505
Tuwachambue wachambuzi wetu wa soka
Nasikia wanaingia sana JF kusikilizia pale tunapo wachambua na wao

Mimi naanza na wachambuzi wa Clouds Media haswa Sports Extra

WAONGOZAJI ni
Prisca Kishamba
Alex Lwambano
Mkazuzu

WACHAMBUZI
Shafii Dauda
Edgar Kibwana
Coutinho
Yahaya Njenge
Amri Kihemba
Privaldinho
Faram Kihamwe
Issa Marda
James Turpa Turpa

RIPOTA
Mkomwa

Kwa waongozaji sina neno nao sana wanajitahidi ingawaje Prisca anaoneka mweupe kiaina na Lwambano ni mswahili sana(anafurahisha) yaani huwa anawakilisha mawazo ya wale mashabiki wa kawaida kabisa kwa jinsi anayofanyaga assumptions zake

WACHAMBUZI
Privaldinho
Itoshe tu kusema hamna kitu pale zaidi ya kuremba remba sauti na ujuaji
Haka kajamaa bora kaende tu kwenye field yake ya sheria, huku miyeyusho sana

Coutinho
Huyu anaijua vizuri sana basketball na yuko vizuri kuichambua
Ni mmoja wa wachambuzi wa ki theory zaidi kuliko FACTS, anaonekana yupo vizuri ila anakuaga bias linapokuja swala la Liverpool

Edgar Kibwana
Mzee wa what a game, what a come back, what a goal[emoji23][emoji23]
Huyu bwana kwa kutaja kiufasaha majina ya vilabu haswa vya italiano mbona utampenda
Kiujumla ni mjanja mjanja flani hivi kwenye uchambuzi na ana vitakwimu fulani hivi



Yahya Njenge, Farahn Kihamwe na Issa Maeda
Hawani ni aina ya wachambuzi wa kujenga sana theory kuliko uhalisia
Wakianza porojo za kwa nini Simba haifungi yaani atatengeneza equation, formula, ikapanda ikashuka sijui mfumo tactical effect yaani blah blah mingiiiii

Amri Kiemba
Huyu ndio mtu pekee pale clouds media anajua kuchambua mpira wa miguu kwa FACTS au Professional opinion.
Ligi ya kibongo anachambua kwa fact haswa nakitaalamu bila kuvuta maneno mengii, anakua mtamu zaidi muongozaji akiwa Lwambano halafu aanze kumchagiza kuhusu ligi za bongo na figisu zake

Shaffi Dauda
Mzee wa controversial
Ujuaji mwingii
Anaweza akatoa mtazamo wake bongo nzima ikasimama kumjadili, akina Manara wataitisha hadi na media
anajitahidi kiasi chake

James Turpa Turpa[emoji23][emoji23]
Huyu jamaa ni comedian
Kama unataka kupata habari za michezo kikomedi basi huyu jamaa atakufaa

Mkomwa
Huyu mshkaji ni ripota mzuri sana kwenye vijiwe vya maahabiki na wauza magazeti

Nini maoni yako?
 
Hebu tupe tathimini ya

Oscar Oscar
Jemedari saidi
 
Mchambuzi wa Ukweli anaejua mpira ni Dua Said, Lunyamila, na wakongwe wengine kama mshapata bahati wakialikwa hawa wanajua wengine full midomo utopolo, Shafii anashida ya kujifanya anajua kuliko wengine anapenda kusikilizwa sana yeyw kuliko kusikiliza ya wengine. Akiwa maikilizaji pia mzuri ataimarika zaidi.
 
Prisca kishamba empty head pale, yeye ni kuiongelea akaunti yake tu instagram sijawahi mkubali,nilimuonea huruma siku moja tu manara alivyomtoa nduki..Priva abiud anapenda kudakia story,mwenzie hajamaliza kuongea naye anaongea,thanks kwa kiemba uwa anamshushua kwa facts. Kibwana anajua sana

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Kuchambua mpira ni sanaa na kucheza ni kipaji sio lazima ucheze ili uchambue mpira, naona muhimu ni uwe na uelewa wa kile unachozungumzia

Nikweli sio lazima uwe kocha au mchezaji ili uje kuwa mchambuzi

Lakini iwapo kutakua na wachambuzi wawili wazuri sana basi yule aliyecheza mpira atapunguza sana nadharia na kuangalia zaidi uhalisia

Mtu kama Kiemba ukimkinganisha na Edgar Kibwana au Coutinho utaona akina Kibwana wanajua vitu vingi sana kuliko kiemba
Lakini Kiemba au Mayai watachambua kwa fact rahisi kabisa mimi na wewe kuelewa kuliko akina Coutinho ambao mbaka wa google kwanza
 
My list.
1 Tigana Lukinja
2. Ally Mayai Tembele
3. Ally Kamwe
4. Dominick Salamba
5. George Ambangile
6. Theovinist Alex Kashasha RIP
7. Salma Ngale
8. Wachambuzi wa ZBC yule bonge white na mwingine tall ana sura kama mkenya hivi, kwenye michuano ya CAF wanafanya poa sana.
 
Kwa waongozaji:
1. Alex Lwambano (Clouds FM)
Jamaa anajua kuiteka hadhira. Huongea kwa lugha rahisi na uchagizaji wake huwakilisha maoni ya mashabiki wengi wa mpira. Namkubali sana.

2. Maulid Kitenge (E FM)
Mwamba anajua, ana vionjo vingi vya kumteka msikilizaji. Namkubali ila siku hizi kapungunza utulivu kidogo.

3. Tunu Hassan Shenkome ( E FM)
Mdada yuko vizuri, huleta mada flani tata ambapo akina Oscar huingia kichwakichwa! Namfananisha na Lwambano kwa clouds.

5. Prischa Kishamba (Clouds FM) .. wa kawaida.

6. Mwanaidi Suleiman (Wasaf FM)
Huyu amna kitu kabisa zaidi ya kuchekacheka.

7. Yusuf Mkule (Wasaf FM )
Anajitahidi ila bado ana mengi ya kujifunza, pia apunguze kumuiga Kitenge.
 
Kwa wachambuzi.

Wakali wangu ni hawa.
1. Mwl Kashasha (RIP)- TBC
2. Amri Kiemba -Clouds
3. Jeff Leah - E FM
4. George Ambangile - WASAF FM
5. Eddo Kumwembe - WASAF FM
Huyu hana maneno mengi ila anaeleweka ( Short and clear)
6. Ally Mayai -Azam Tv

Wabovu wangu:
1. Oscar Oscar - E FM
Huyu hutumia nguvu nyingi

2. Jemedari Said E- FM
Hutumia nguvu nyingi kueleweka

3. Ibrahim Masoud - E FM
Ana ujuaji mwingi

4. Shaffih Dauda - Clouds
Mjuaji na hutumia nguvu nyingi

5. Salama Nghale - U FM
Anabebwa na jinsia yake, uwezo wa kawaida sana. Ni mweupe kichwani kama Prisca Kishamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…