Wachawi mliopo JF nitoleeni ufafanuzi wa hiki kilichonitokea usiku.

Pacbig

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2017
Posts
1,095
Reaction score
2,087
Kwanza poleni na majukumu ya kusaka ugali wakuu.JF ni mtandao unaotukusanya watanzania na wasio watanzania wenye kazi,sifa,itikadi,fikra,mitazamo na karba tofauti tofauti.Humu kuna walimu,wahandisi,Madaktari,Machangudoa,Wanasheria,Wanasiasa,Wadananda,Mapaparazi etc

Leo ninawaomba wachawi wote mliopo humu JF mnisaidie kunitolea ufafanuzi wa kilichonitokea leo usiku.

Mimi ninasoma chuo fulani huku Tanga nimepanga chumba kimoja katika nyumba ambayo ninaishi na baba mwenye nyumba na familia yake .Leo usiku nikiwa nimelala sikujua ilikiwa ni saa ngapi.Nikiwa kama niko usingizini nilihisi kama kuna mtu kalala pembeni yangu,nikashituka nikanyoosha mkono nikajikuta namushika sehemu za makalio yalikuwa kama ya mwanamke(japo sina uhakika).Nilipomshika akawa kama kasogea mbele kidogo,nilikuwa nimelala kifudifudi sekunde chache baadae ikawa kama kuna mikono ipo shingoni mwangu inanigandamiza kwenye godoro,Pia kuna kama moto fulani ambao hauunguzi sana unanichoma maeneo ya kuanzia kichwani hadi mgongoni.

Kilichonishangaza zaidi viungo vyote vya mwili vilikuwa havina nguvu nikijaribu kuitoa ile mikono ya Yule mtu,mikono yangu haiwezi hata kunyanyuka.Nikijaribu kugeuka mwili hauna nguvu kama umegandishwa.Miguu pia hainyanyuki.Nikitaka kuongea mdomo nao hauwezi.Ni macho tu ndio yalikuwa yanafumbua.Nilikuwa nikifikiria labda niko ndotoni lakini najiona sipo ndotoni kabisa ni kitu real.Baada ya dakika kadhaa nilishituka yaani hata sielewi vizuri nikajikuta nipo katika hali ya kawaida tu.

Nawaulizeni nyinyi wachawi je hivyo ndivyo mnavyoroga na ndivyo mnavyofanya michezo yenu au ni mawenge yangu tu.

Wachawi karibu.
 
Hakuna uchawi apo ngoja wataalamu waje wa kukufafanulia vizuri
 
Tukisema okokeni mnasema hakuna kuokoka duniani, tukisema mwaminini Yesu mnasema ukristo ni dini yawazungu, cye tuliookaka hatukani nambo ya namna hiyo, kabla cjaokoka niliteswa sana wachawi kwa namna hyohyo, bat today I thanks God through Jesus Christ nau niko huru, Mwamini Yesu mkuu nawe utaokoka nakadhia hiyo.
 
Sawa mkuu ila ngoja nikurekebishe kidogo umeongoka na sio kuokoka...
 
Huu Uzi ni ngumu kuchangia...maana na ww utaonekana walewale..jasiri amfafanukie mkuu [emoji16][emoji23][emoji124][emoji124]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…