MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Miaka ya nyuma ilikuwa ni nadra sana au ilikuwa hamna kabisa mchezaji ligi kuu Uingereza aliokuwa na uwezo wa kuwasiliana kwa lugha adhimu ya kiswahili, miaka imeenda na mambo yamebadilika wachezaji kibao sasa EPL wanaongea kiswahili kuliko hata Mbwiga Mbwiguke.
Hii ni baadhi tu ya wachezaji siku ikitokea umekutana nao usiwaambie "Hawa yuu mai bosi?" bali waambie "Mambo ni yanaendaje jamaa yangu?".
1.VICTOR WANYAMA.
Mchezaji wa kimataifa kutoka Kenya anayechezea timu ya Tottenham Hotspurs ya London anaimudu vilivyo lugha ya Kiswahili hata kupewa ubalozi wa lugha hiyo na chombo rasmi kinachohusika na ukuzaji wa lugha hiyo nchini Kenya. Kiswahili ni lugha rassmi ya mawasiliano nchini Kenya sambamba na Kingereza huku idadi ya Wakenya wanoongea kiswahili fasaha ikiizidi ile wanaoongea kingereza fasaha.
2.DIVOCK OKOTH ORIGI
Mchezaji huyu wa Ubelgiji na klabu ya ligi kuu ya Liverpool ya nchini Uingereza na mtoto wa mchezaji w zamani wa timu ya taifa ya Kenya Mike Origi pia ni mmoja ya wachezaji wanaoimudu vyema lugha ya Kiswahili. Origi aliyeanza kukipiga katika klabu ya Genk ya Mbwana Samatta na kuiwakilisha Ubeligiji katika kombe la dunia mwaka 2014 anasema Kiswahili ndio lugha pekee ambayo amekuwa akiwasiliana na baba yake na familia ya upande wa baba yake nchini Kenya toka akiwa mtoto mdogo.
3.KELVIN DE BRUYNE
Mtoto wa Herwig na Anna, Kevin De Bruyne ametumia muda mwingi wa utoto wake Ulaya na Afrika. Mama yake Anna mzaliwa wa Burundi ambaye katika wakati fulani wa machafuko aliwahi kuishi Kigoma na Dar es Salaam nchini Tanzania na Ivory Coast. Kevin ambaye anaongea Kifaransa, Kidachi na Kiiengereza pia anakitaja kiswahili kama lugha anayoilewa kwa kiasi cha kuwasiliana vizuri.
4.LUKAKU, KOMPANY NA MICHY BATSHUAYI
Pamoja na kuzaliwa nchini Ubeligiji kwa wazazi wahamiaji wenye asili ya Kongo, wachezaji hawa kwa pamoja na kwa wakati tofauti wanadai wanaongea Kifaransa, Kiingereza na Kiswahili. Lukaku anakipiga Manchesster United, Vincent Kompany akichezea Manchester City na Michy Batshuayi akichezea klabu ya Valencia akitokea Chelsea kwa mkopo.
5.CHRISTIAN BENTEKE
Christian Benteke, alizaliwa 1990 Kinshasa nchini Kongo ambapo ambapo mwaka 1992 yeye na familia yake walihamia mkoa wa Rukwa nchini Tanzania ambapo walikaa mpaka mwaka 1996 kabla ya kuhamia nchini Ubeligiji. Benteke anavitaja Kiswahili na Kilingala kama lugha yake ya kwanza,huku pia akisema ana uwezo wa kuongea Kifaransa na Kingereza kama lugha yake ya pili. Benteke ana haki ya kuchezea timu ya Kijamhuri ya Kongo kama nchi yake ya kuzaliwa lakini anapendelea zaidi kuchezea timu ya Ubeligiji ambapo pia anatajwa kutaka kutimkia Fulham dirisha la usajili kukwepa benchi la Crystal Palace.
Chanzo: SpotiKona..