lil wayne
JF-Expert Member
- Apr 15, 2016
- 992
- 904
Wasaalam wanajamvi!
Leo ninapenda kuwaletea 'Unabii' mwanana kabisa kuhusu vijana hawa wanaochezea klabu ya Simba SC.
Kama ilivyo desturi ya soka la Tanzania na pia hali halisi ya Vilabu hivi hasimu vya Jijini Dar es Salaam yaani Simba SC na Yanga SC.
Kuna baadhi ya vijana mashuhuri ambao ninaona kabisa kuwa hawatoweza Maliza soka lao Bila kuitumikia Klabu kubwa kabisa na yenye Mafinikio makubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki yaani Dar es Salaam Young Africans SC.
Hii ni kutokana na Kiasi cha Kiu ya Mafanikio waliyokuwa nayo vijana hawa wa Klabu ya Simba SC. Ndoto niliyonayo inanionyesha dhahiri kuwa watachezea klabu yao hiyo ya sasa kwa muda mrefu bila Mafanikio ya kuwaridhisha na hapo ndipo watakapo amua kuwa Mahala pekee ambapo wanaweza pata mafanikio ya kisoka ni Dar es Salaam Young Africans SC.
Kama inavyo julikana kuwa Yanga SC ni kisima cha NDOTO kwa kila mwanasoka wa kitanzania, hapa ndipo mahala au klabu pekee ambapo mchezaji anaweza kuweka Legacy yake na ikatambulika katika kipindi cha Maisha yake yote.
1. Tshabalala/ Zimbwe Jr -
Kuhusu Huyu dogo sina hata la kuzungumzia, nani hamjui beki kisiki wa zamani wa Yanga SC Said Zimbwe Mwaibane. Naam huyu dogo ukimchanja kidogo tu anatoa damu yenye rangi ya Kijani, au usaa wa njano. Hawezi kufikiria mara mbili kama akiamua kufuata Mafanikio kwenye klabu aliyochezea mjomba yake.
2. Ibrahim Ajib -
huyu ni kijana mchapa kazi sana akiwa uwanjani. Na hakuna anayebisha hilo. Ila mapungufu yake ni kwamba ndiye mchezaji ambaye si hodari mno kwenye kutupia ndimu kambani, licha ya kuwa ni mchezaji mshambulizi. Naona kabisa akitumikia Klabu ya Simba kwa muda kabla hajaamiza vilago vyake na kuhamia Jangwani pale atakapo tambua kuwa alipo hapamuwezeshi kubeba ndoo.
3. Shiza Kichuya -
Huyu dogo nimekuwa nikimkubali tangu alipokuwa Mtibwa Sugar. anauwezo mkubwa sana. Ila sioni kama atafanikiwa pale alipokuwa sasa yaani Simba. Maana ana aina ya soka ambalo haliko Compatible na soka la klabu anayoitumikia kwa sasa... Licha ya kuwa amefunga mabao mengi. Naona ana nafasi kubwa sana pale Jangwani ambapo ndio Klabu pekee yenye utamaduni wa kutumia winga kama mhimili mkuu wa ushindi. Ni kweli dogo anafurahia pale alipo kwa sasa. Ila haita chukua muda mrefu sana mpaka aje kutambua kuwa anahitaji Mafanikio ambayo anaweza siku moja akakaa na kuwahadithia wajukuu zake kuwa aliwahi kucheza soka na kupata hiki na hiki. Sioni kama naye anaweza dumu sana pale Msimbazi.
VIELELEZO:
Ninapo sema Yanga SC ni klabu yenye utamaduni wa kujali mafanikio zaidi sidanganyi. Hebu niambie ni mchezaji gani aliyekimbia Msimbazi na kuja Yanga SC kwa ajili ya Mafanikio akayakosa?
1.Mcheki Yondani,
2.Mcheki Barthez,
3.Mcheki Tambwe,
4.Mcheki Deogratius Munishi
5.Mcheki Twite (Baada ya kuambiwa kuwa asaini Jangwani penye kumuwezesha kupata mafanikio na aachane na kusaini simba),
6.Mcheki Ngassa baada ya kuitumikia Msimbazi kwa Mkopo akaona isiwe tabu arudi Jangwani na msimu huo huo akabeba ndoo ndio akatimkia South.
7. Mcheki Hassan Kessy atakavyotimiza ndoto yake msimu huu wa 2016/17
Ni mchezaji gani ametoka Yanga SC kwenda Simba SC kutafuta Mafanikio.?
Karibu Ibrahim AJIBU,
Karibu Mohammed 'Zimbwe Jr' Hussein, Karibu Shiza Kichuya.
Njoeni Dar es Salaam Young Africans SC mtimize ndoto zenu kabla uzee wenu hauja wazuia kuyagusa mafanikio yenu
Nawasilisha!!!