Wachezaji Leicester City Wawasili Thailand Kumzika Mmiliki wa Klabu

Wachezaji Leicester City Wawasili Thailand Kumzika Mmiliki wa Klabu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
104166415_hi050383194.jpg



Wachezaji wa Leicester City wamewasili nchini Thailand kwa mazishi ya mmiliki wa klabu ambaye alifariki kwenye ajali ya helikopta. Jamie Vardy na nahodha wa klabu Wes Morgan ni baadhi ya wachezaji ambao wamehudhuria mazishi ya Vichai Srivaddhanaprabha kwenye hekalu mjini Bangkok. Mazishi hayo yaliyoanza Jumamosi yataendelea kwa wiki nzima. Helikopta hiyo ilianguka baada ya kupaa kutoka uwanja wa mpira wa klabu hiyo tarehe 27 Oktoba na kumuua Vichai na wengine wanne.


104167640_hi050383590.jpg



Wachezaji wa Leicester walisafiri kwenda Thailand kwa safari ya saa 12 Jumamosi baada ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Cardiff kenye ligi ya Premier, mechi yao ya kwanza tangu Vichai afariki. Meneja Claude Puel amewangoza wachezaji wake kwenye mazishi hayo.
104159003_hi050356759.jpg



Nusara Suknamai, Kaveporn Punpare, rubani Eric Swaffer na mpenzi wake, Izabela Roza Lechowicz, nao walikufa kwenye ajali hiyo. Mazishi ya Bi Nusara yalifanyika Bangkok Jumamosi.


Bi Nusara 32 mmoja wa wafanyakazi wake Vichai alichukua nafasi wa pili kwenye shindano la urembo la mwaka 2005 la Miss Thailand Universe.


104166411_hi050367344.jpg



104159007_hi050358649.jpg



104165613_hi050382273.jpg



104165617_hi050367338.jpg



104167644_hi050383668.jpg



104129992_afp-gettyhi050237613.jpg
 
inahuzunisha kweli, pole sana kwa walioguswa na wapenzi wa soka kiujumla
 
Aisee acha ule ukanda una madon wa kutisha sana humjui Thaksin Shinawatra
 
"
Bi Nusara 32 mmoja wa wafanyakazi wake Vichai alichukua nafasi wa pili kwenye shindano la urembo la mwaka 2005 la Miss Thailand Universe."

Huyu Miss alikuwa mfanyakazi wake kweli ? Basi sawa

R.I.P
UKIFIKA NAWEWE UKO UWAULIZE
 
R I P Vichai
Your surname /family name is cumbersome to me.
See you in glory!
 
Kwa wajuzi wa kithailand mtusaidie hili jina jinsi linavyotamkwa:- "Srivaddhanaprabhar"
 
Back
Top Bottom