DOKEZO Responded Wachezaji Pamba Jiji kususia Mechi ya mwisho wa Ligi Kuu sababu hawajalipwa kwa miezi mitatu!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
​

Wachezaji wa Pamba Jiji FC wametishia kususia mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union wa Juni 30, 2026, kutokana na kile walichodai kuwa ni kucheleweshewa malipo ya mishahara na bonasi kwa zaidi ya miezi mitatu.

Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zinaeleza kuwa hali ngumu ya kifedha imeendelea kuwaathiri wachezaji na benchi la ufundi, huku wakidai juhudi za kutafuta ufumbuzi kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo zikiwa hazijazaa matunda.

Mmoja wa wachezaji, ambaye hakutaka kutajwa jina lake, amesema wamekuwa wakiahidiwa kulipwa bila mafanikio, hali iliyosababisha kushuka kwa morali ndani ya kikosi hicho.

Tumechoka kuahidiwa kila mara. Mishahara na bonasi hatujalipwa kwa muda mrefu, viongozi wengi hawapatikani na hali imekuwa ngumu kwa wachezaji. Tunaendelea kulaumiwa na mashabiki wakati changamoto zetu hazijapatiwa ufumbuzi, ~ alisema mchezaji huyo.

Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kuhusu changamoto za kiutawala na kifedha ndani ya klabu hiyo yenye makao yake jijini Mwanza, huku baadhi ya wadau wa soka wakitaka hatua za haraka zichukuliwe ili kulinusuru kundi hilo.

Hadi sasa, uongozi wa Pamba Jiji FC haujatoa taarifa rasmi kuhusu madai hayo ya wachezaji wala kuhusu hatma ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union.

Majibu ~ RC Said Mtanda: Ni kweli Wachezaji wa PAMBA JIJI wanadai mishahara ya miezi mitatu, watalipwa soon, nimewatafutia mshahara wa mwezi mmoja kwanza
 
Ni kawaida yao alafu mechi ya mwisho inauzwa wanapata chochote kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…