Wachezaji wa African Lyon wadai Mohamed Fakhi hakupewa kadi ya njano

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Mechi ya Kagera Sugar na African Lyon ndiyo inayoleta utata kwa sababu ndiyo inayo mhukumu mchezaji huka kwamba ndiyo ilikuwa mechi ya tatu mfululizo anaoneshwa kadi ya njano.

Mechi hiyo hiyo ndio Kagera wanasema mchezaji hakuoneshwa kadi lakini wanakubali kuwa kabla ya mechi hiyo ni kweli alikuwa na kadi mbili za njano.

Mechi hiyo haikuoneshwa na Azam TV wala haikurekodiwa,Kwa upande wao Kagera Sugar wanasema kwenye rekodi zao hakuna hiyo kadi inayolalamikiwa na Simba.

Kwa utafiti uliofanywa na Shaffih Daudi kwa baadhi ya wachezaji wa African Lyon waliocheza mechi dhidi ya Kagera Sugar wanasema hawakuona tukio lolote alilofanya Mohamed Fakhi lililopelekea kuoneshwa kadi ya njano na hawakuona mwamuzi akimuonesha Fakhi kadi ya njano.
 
huo ni uzembe tu kwani hakuna taarifa za waamuzi?waamuzi wapo watano kuanzia mwamuz wa kati,waamuzi wawili wasaidizi,kamisaa wa mchezo,na msimamizi wa kituo wote hawa wasilione hilo tukio? acheni ubabaishaji bhana huku ni kuzionea timu ndogondogo na kukatisha tamaa wachezaji km MTU kashinda kwann mbadilishe Matokeo? huko ni kufanya siasa za mpira sasa cha kagera na afrikan waliocheza wanasema hakuna kadi yoyote huu ni usanii tu unafanyika
 
Namshangaa sana Shafii Dauda. Sasa hivi ni kiongozi wa soka na sio shabiki wa mpira. Badala ya kufanya ufuatiliaji makini wa taarifa kama hiyo yeye analeta ushabiki maandazi. Hebu jiulize Ripoti ya Kamisaa na Ripoti ya Refa zote zipo mikononi mwa wahusika tokea mechi ilipochezwa. Leo anaibuka mtu na viroja na sio hoja anataka watu waamini kile asemacho ili kutengeneza futbolifitna. Pole sana atafute wa kudanganya.
 
Duh, hili suala kumbe rekodi hazipo?

Kweli mpira wetu uko katika hali mbaya ya kiutawala hadi kufikia watu kuulizana kumbukumbu muhimu kama hizi kupitia uwezo wao wa kukumbuka kiakili?

Kama ni hivyo basi kuna tatizo kubwa kuliko nilivyodhania
 
Shafii Dauda ni mikia mwenzenu, ukiona hadi ameshindwa kudanganya basi nafsi inamsuta.

Hakuna ubingwa wa mezani chezeni mpira matokeo yanapatikana uwanjani na si mezani.
 
Hadi sasa point 3 zilizopewa simba tayari zimesharudishiwa kagera sukari
 
Ni kweli waweke mambo hadharani kwann wafiche watafutwe makamishina waliosimamamia mchezo huo
 
Hivi wanaodai hizo points ni kagera kweli au PEREGE FC?haiingii akilini...hao kagera wadai points wao wanataka UBINGWA?AU WANASHUKA DARAJA?yote KAMBARE FC hao....ndy maana mnakula 4 G sababu ya kufuatilia ya watu
 
Hivi wanaodai hizo points ni kagera kweli au PEREGE FC?haiingii akilini...hao kagera wadai points wao wanataka UBINGWA?AU WANASHUKA DARAJA?yote KAMBARE FC hao....ndy maana mnakula 4 G sababu ya kufuatilia ya watu
Yani leo Simba imefikia hatuwa ya kulilia point ambazo ilishindwa kuzipigania uwanjani? Too sad.

Sasa inabidi club yenu ihamie kwenye kubet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…