Wachezaji wa jadi ardhi sports watakiwa kujiamini katika mashindano ya Shimiwi 2026

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165


Mwenyekiti wa Ardhi Sports Club, Bw. Swagile Msananga, amewataka wanamichezo wa Michezo ya Jadi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutumia ujuzi walioupata, kucheza kwa utulivu na kujiamini katika Mashindano ya SHIMIWI 2026, akisisitiza umuhimu wa kila mchezaji kutambua uwezo wake katika kuwania ushindi.

Amezungumza hayo Septemba 25, 2026, katika kikao cha tathmini kilichofanyika katika Ukumbi wa Moshi Club , akisisitiza kuwa kila mchezaji kupambana kwa uwezo wake na kujiona kuwa mpinzani katika kila mchezo.

Bw. Msananga amewataka wanamichezo hao kuweka juhudi katika kuhakikisha wanarejesha vikombe katika Wizara, ili viongozi wa Wizara waone matokeo ya ushiriki wao katika mashindano hayo, Aidha amewatakia maandalizi mema na mashindano yenye mafanikio, akisisitiza umuhimu wa kutumia ujuzi walionao ili kupata ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, Bw. Benedict Mwombeki, ameahidi ushindi mkubwa na kusisitiza kuwa kila mchezaji anatakiwa kuweka ndoto ya kufika fainali, akieleza kuwa kufika hatua hiyo ndiyo sehemu muhimu inayomfanya mshiriki kuitwa mshindi.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Ardhi Sports Club, Bi. Neema Mwenge, Mwalimu wa Michezo ya Jadi Bw. Abdulhafidhu Mohamed, Mratibu wa Michezo ya Jadi, Bw. Hijja Chande, pamoja na wanamichezo wa Michezo ya Jadi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mashindano ya Michezo ya Jadi yanatarajiwa kuanza Septemba 27, 2026, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa michezo ya SHIMIWI 2026. Michezo hiyo inajumuisha Karata, Drafti, Bao, Darti, Riadha,na Kurusha Tufe .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…