Wachezaji wa kigeni

Multdealer

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2019
Posts
226
Reaction score
232
Habari,

Jana nilikuwa nafuatilia hafla fupi ya miaka miwili ya uongozi wa TFF chini ya Rais Wallace, mengi yalizungumzwa ila kuna jambo moja mimi binafsi sijakubaliana nalo jambo lenyewe ni hii dhana:

Yakwamba wachezaji wa kigeni ni lazima wacheze timu za taifa wanapo toka na pia idadi ya wachezaji hao ipunguzwe,wakati huo huo sisi tunapiga debe wa kwetu watoke waende kwa wenzetu.

Sasa na nchi za wenzetu wakiweka vigezo hivyo ina maana kuna wachezaji wengi wa Tanzania watakosa nafasi ya kupata exposure nchi nyingine.

Kwa mfano, Highland itamtema Banda, wakina Emily Mgeta watatemwa huko Ujerumani na wengine wengi ambao wapo nje.

Mimi ninachoona wachezaji wakigeni waje tu, atakaye shindwa kuendana na kasi ya ligi ataonekana na ataachwa na klabu husika.

 
Hawa huwa wanaiga sababu timu ya taifa inachukuwa wachezaji wachache mno kwa hiyo si kila mchezaji anapata bahati ya kuchezea timu ya taifa.
 
Wapunguzwe tu na ikibidi turudi kule kule, wasizidi watano! Hii itapunguza viongozi wa timu na makocha wao kusajili wachezaji wengi magarasa ili kupata tu 10% kama ilivyo sasa.
 
Itakuwaje kama mchezaji kipindi kasajiliwa yupo katika national team, wakat akiendelea na mkataba akatemwa na timu ya taifa.. Je TFF watazilazimisha timu kuvunja mkataba
 
Itakuwaje kama mchezaji kipindi kasajiliwa yupo katika national team, wakat akiendelea na mkataba akatemwa na timu ya taifa.. Je TFF watazilazimisha timu kuvunja mkataba
Hili nalo ni jambo la kujiuliza
 
VPL pekeake ina timu 20 zenye wachezaji 30 @ na kufanya idadi ya wachezaji wote VPL kuwa 600!

Ktk VPL, vilabu vyenye FINANCIAL MUSCLES ya kusajili wageni ni AZAM, SIMBA na YANGA, kidooogo na KMC!

Jumla ya wachezaji wa kigeni ktk Vilabu vyote vya VPL haifiki 100! So bado kuna pool kubwa ya kupata wachezaji wa National team!

Mtibwa Sugar haina hata foreigner mmoja ktk kikosi chake, je imetoa wachezaji wangapi ktk National team CHAN?
 
Nafukiri TFF kabla ya kupitisha makatazo kama hayo,Inabidi wawe wana jiuliza maswali kama haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…