Wachezaji wa Simba wamelewa pesa

Wachezaji wa Simba wamelewa pesa

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika ngozi nyeusi ni nyeusi hata uifanyie jema gani. Wachezaji wa Simba ndio wanaoongoza kulipwa pesa nyingi na uongozi wa klabu ya Simba kuliko klabu yoyote Tanzania.

Kutokana na kulipwa huko, wachezaji hao wamelewa pesa hali ambayo wamesahau majukumu yao. Wachezaji wamekuwa hawajitumi uwanjani, hawaangalii gharama kubwa zinazotumika juu yao matokeo yake ni kucheza chini ya viwango.

Angalia mechi ya Simba na Yanga walishindwa kujituma mpaka magoli yakaruďishwa, ni aibu. Leo huko Zanzibar wachezaji hawakujituma kabisa hali ambayo imemfanya Mwenyekiti wa Bodi ajiuzulu.

Ushauri: Iundwe Kamati iwachunguze wachezaji wote waliocheza chini ya viwango vyao katika mechi zote mbili kisha WAFUKUZWE, hatuwezi kuwa na wachezaji wanaolipwa pesa nyingi lakini HAWAJITUMI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom