Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
- Thread starter
-
- #21
Tukianza na mabeki wakuachwa ni shomari kapombe- huyu ni injury prone sana hawezi kuendana na soka la mikikimikiki,
wawa- huyu umri ushamtupa naona ligi ya mabingwa atakuwa uchochoro pamoja na shabalala -ambaye nae sio mzuri kwenye ukabaji kitu ambacho anakosa sifa ya ubeki
Erasto nyoni- siku hizi hata namba hapati kiwango kimeshuka Mara sabini huyu ni wakuachwa kwani anasababisha faulo zisizo na msingi ambazo zitatukosti huko mbeleni
Tukija kwenye viungo wakuachwa pale simba ni pamoja na wafuatao:
Luis miqquesone- huyu dogo anapoteza sana mipira atatukosti sana tukikutana na timu mzuri hasa waarabu na ukizingatia umbile lake haliruhusu
Kahata- huyu jamaa bado sana naona hajafiti kwenye mfumo kwani anashindwa kufanya kile ambacho watu walitarajia na tatizo lake kubwa ni pasi zake mbovu
Chama- hapa naona wengi watanipinga lakini jaribu kuangalia kwa jicho la tatu huyu jamaa ndo naona anaikosesha simba magoli mengi sana kwani anakawaida ya kukaa sana na mipira badala ya kuwaangalia wenzie awapo kwenye third ya mwisho ya uwanja
Tukija kwenye washambuliaji
Kagere- huyu jamaa ni wakupitishiwa fagio kwani siku za karibuni amekuwa kwenye kiwango kibovu sana na ukizingatia umri nao ndoivo tena
John bocco- huyu mtu hapana aisee yani kwenye nafasi kumi anapata moja sasa itakuwaje tukikutana na Esperance ambapo tutapata nafasi moja tu.. ili simba iweze kufanya vizuri kimataifa iachana na bocco itafute mshambuliaji mnyambulifu
Duuh sawa mkuu, tunaheshimu mawazo yako