Wachezaji wa Taifa Stars tumieni vizuri mashindano ya AFCON. Vizazi Vijavyo Vitawashukuru na Kuwakumbuka

Wachezaji wa Taifa Stars tumieni vizuri mashindano ya AFCON. Vizazi Vijavyo Vitawashukuru na Kuwakumbuka

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Nimewaza ni nafasi gani hii adimu sana ambayo wachezaji wa Taifa Stars wamepata ya kuonekana kuonyesha vipaji vyao. Nikasema kweli Mungu hamtupi mja wake!

Platform kubwa kama hii wachezaji wa michezo mbalimbali wanaojitambua walipoipata waliitumia ipasavyo kuonyesha mambo mbalimbali ambayo labda taifa au dunia haiyapi kipaumbele inavyostahili. Kuna mambo ya unyanyasaji wa kijinsia, uhuru wa kujieleza, ukandamizaji na uonevu unaofanywa na wenye mamlaka na nguvu, haki za binadamu, nk.

Nikawakumbuka wachezaji mbalimbali duniani, tena wakubwa tu na wenye vipaji vya hali ya juu ambao walikuwa na vingi vya kupoteza (mali, mikataba minono, kazi zao, mashabiki, nk.). Hao walitumia nafasi hizo kufanya maamuzi haya na mpaka leo na labda hata milele, dunia itaheshimu kujitoa kwao kwa ajili ya wengine.

Kufanya mambo haya inahitaji kuweka ubinafsi pembeni na kuangalia mahitaji ya wengi na pia vizazi vijavyo. Hawa watu hawakurubuniwa kwa mikataba minono au ahadi za viwanja kule Washington DC au New York.

Kuna hadi walioenda jela kama Muhammad Ali, lakini leo hii ukitaja wanamichezo waliowahi kuheshimika duniani hawezi kukosa.

black power salute at the olympics.jpg
Derick Ross, Lebron James and Kobe Bryant.jpg
ethiopian athlete.jpg
Kapernick kneeling.jpg
muhammad ali.jpg
NBA.jpg
serena williams.jpg
soccer.jpg



Nawakumbusha tu historia inavyoandikwaga.
 
Tanzania 3 - 0 Uganda : 23rd March 2019. Taifa Stars qualify for the Africa Cup of Nations AFCON 2019 finals in Cairo, Egypt



Source: Bongo Zozo
 
Back
Top Bottom