Wachezaji wa Yanga enzi za sekilojo rafiki yenu niliyekutana naye Denmark anawasalimia sana

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
8,082
Reaction score
17,838
Mzuqa

Nililetaga uzi wa huyu jamaa miaka miwili iliyopita kwenye ID yangu pendwa ya Copenhagen mods wakaipotezea faster.

Ngoja niirudie.

Ni hivi summer 2016 jumamos flani nakumbuka ilikuwa pride day siku ya hawa mashoga wanasheherekea. Nilikuwa kwenye park. Sasa nikataka picha nikawaona jamaa wawili afrika nikawaomba wanipige picha na simu yangu. Mmoja akakubali.

Baada ya kunipiga picha nikamuuliza where are you from akanijibu Ghana. Naye akaniuliza nikamuambia Tanzania jamaa alishtuka akasogea karibu nakuanza kunisimulia.

Yeye alikuwa mchezaji mpira proffessional Ghana. Miaka ya 90 aliichezea costa de sol ya msumbiji. Yanga ilienda maputo kuchuana na CD. Baada ya mechi huyu jamaa walijenga urafiki sana na wachezaji wa Yanga hadi leo anawakumbuka kwa majina Sekilojo Chambua, Ally Mayai, Salvatory Edward, Lunyamila, bakari malima alinichekesha akijaribu julitafuta jina la huyu mchezaj baadaye akalipata Wazir Maadhi that fat boy he used to be quiet and keeping for himself je mnaomjua wazir maadh alikuwa hivyo?

Yanga walivyokuwa wanarudi bongo wakaongozana naye hadi Dar. Anasema hajawahi kuona ukarimu maishani mwake kama alioonyeshwa na wachezaji wa Yanga na wenyeji wake Dar. Yani hasahasa anamsifia sana Ally Mayai alikuwa naye Benet.

Yeye anajiita Charles lakini siyo jina lake halisi ni muislam anajina la kiislam japo hakutaka kuniambia ila nilimuelewa kwasababu alijilipua ujerumani wakamnyima asylum akaja Denmark kujaribu ila walimrudisha tena ujerumani washughulikie kesi yake. Tulipoteleana kidogo ila jana nashangaa jamaa kanitafuta kwenye FB nakuniuliza salam zangu uliwafikishia akina Ally Mayai?

Wachezaji wa Yanga mlioenda kucheza msumbiji na Costa de Sol 1990s mtakuwa mashahidi wa huu uzi kama mpo jamvini itapendeza sana mkiongezea nyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…