Wachezaji watatu ambao wamebahatika kuchukua Kombe la Dunia kama Wachezaji na wakiwa Makocha

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
2,224
Reaction score
4,472
Ni Watu watatu(3) tu ndio ni watu watatu tu Dunia nzima yani unahesabu 1,2,3 ndio walioweza kuchukua Kombe hili kubwa na lenye hadhi kubwa katika mchezo wa Mpira wa Miguu.
Na ndio maana nikawaita UTATU MTAKATIFU

Wanaume hao ni.
1. MARIO ZAGALLO🇧🇷
Huyu alikua Foward, Mchezaji Raia wa Brazil.
Amebeba Kombe la Dunia kama Mchezaji Mara Mbili(2) ilikua Mwaka (1958) na(1962)
Akabeba kama Kocha Akiwa na Brazil Mwaka (1970)

2. FRANZ ANTON BECKENBAUER🇩🇪
Huyu Alikua Mchezaji Raia wa Ujerumani Ila kipindi hicho inaitwa Ujerumani Magharibi (West German.

Aliiongoza Ujerumani Magharibi kama Nahodha(Captain) kutwaa Kombe la Dunia Mwaka (1974).

Na Mwaka (1990) akaiongoza Ujeruman Magharibi hiohio Kutwaa Taji hilo ila mda huu akiwa Kama Kocha.

3:DIDIER CLAUDE DESCHAMPS🇫🇷
Jamaa flani kama Mpole ila very genius na soka na hilo kalidhibitisha kabisa. Huyu ni Raia wa Ufaransa na ndie Kocha Wa Timu ya Taifa Ya Ufaransa kwa sasa.

Huyu ndie anaekamilisha ule UTATU MTAKATIFU wetu.
Enzi za Uchezaji wake alikua anacheza nafasi ya Kiungo Mkabaji.

Amefanikiwa kutwaa Taji hili kubwa akiwa Mchezaji Mnamo Mwaka (1998) akiwa tena kama Nahodha(Captain) wa Timu ya Taifa wakiwafunga Brazil kwenye Fainali Magoli matatu(3). Akaja akalitwaa Tena Hili kombe Mwaka (2018) mda huu akiwa kama Kocha.

Na Sasa amefanikiwa kufika Fainali Mara mbili Mfululizo tena akivunja Mwiko ambao ulikuepo kwa Takribani zaid ya Miaka 50 zaid kua Bingwa Hajawahi fika Fainali Back to back.

Je, Jumapili hii ataweka record nyingine ya kushinda back to back kama Kocha yuleyule? Ni tusuburi na tuone.
 
Ni Watu watatu(3) tu ndio ni watu watatu tu Dunia nzima yani unahesabu 1,2,3 ndio walioweza kuchukua Kombe hili kubwa na lenye hadhi kubwa katika mchezo wa Mpira wa Miguu...
Aacha record zako za uwongo wewe,usiwe waongea vitu usivyovijua ati "kwa zaidi ya miaka 50 bingwa haijawahi kuingia back to back final'
Hivi Brazil alifanyaje 98?
Ni miaka 50 hiyo toka 98 mpaka 2022?
 
Ni Watu watatu(3) tu ndio ni watu watatu tu Dunia nzima yani unahesabu 1,2,3 ndio walioweza kuchukua Kombe hili kubwa na lenye hadhi kubwa katika mchezo wa Mpira wa Miguu...

Mkuu, unaposema amevunja mwiko wa zaidi ya 50yrs kwa bingwa kuingia fainali back to back mbona unapotosha!??

Brazil 1994 kawa bingwa fainali akicheza vs Italy, kisha 98 kaingia fainali vs France
 
Mkuu, unaposema amevunja mwiko wa zaidi ya 50yrs kwa bingwa kuingia fainali back to back mbona unapotosha!??

Brazil 1994 kawa bingwa fainali akicheza vs Italy, kisha 98 kaingia fainali vs France
Sorry tulia niiweke sawa Erro iliyojitokeza hapo.
Mi nilitaka kusema hakuna Bingwa aliebeba kombe back to back zaid ya Miaka 50 now yani umetoka kubeba then next world cup unabeba tena hicho ndio nilitaka kumaanisha.

#Out of that Furahieni Thread✍️✍️
 
Ni Watu watatu(3) tu ndio ni watu watatu tu Dunia nzima yani unahesabu 1,2,3 ndio walioweza kuchukua Kombe hili kubwa na lenye hadhi kubwa katika mchezo wa Mpira wa Miguu...
Sorry tulia niiweke sawa Erro iliyojitokeza hapo.

Mi nilitaka kusema hakuna Bingwa aliebeba kombe back to back zaid ya Miaka 50 now yani umetoka kubeba then next world cup unabeba tena hicho ndio nilitaka kumaanisha.

Maana naona watu mtakazia kwenye hilo kosa na mtaacha kuangalia dhima kubwa ya uzi huu

#Out of that Furahieni Thread✍️✍️
 
Brazil 94 na fainali 98
 
Kwa mfumo wa uwekezaji wa Ufaransa itasumbua sana ,,maana wao hawaangaiki kutafuta wachezaji wanachukua kwa makoloni yao tu ..
 
Wengi wanaitaja Brazil tu. Baada ya kuanzishwa kombe la Dunia 1930 likichujuliwa na Uruguay Italia ndo ikawa timu ya kwanza kutoka Ulaya kulibeba 1934 na mara ya pili 1938. Ingekuwa England makala za historia zingejaa kila siku.
Good History!✍️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…