Ni Watu watatu(3) tu ndio ni watu watatu tu Dunia nzima yani unahesabu 1,2,3 ndio walioweza kuchukua Kombe hili kubwa na lenye hadhi kubwa katika mchezo wa Mpira wa Miguu.
Na ndio maana nikawaita UTATU MTAKATIFU
Wanaume hao ni.
1. MARIO ZAGALLO🇧🇷
Huyu alikua Foward, Mchezaji Raia wa Brazil.
Amebeba Kombe la Dunia kama Mchezaji Mara Mbili(2) ilikua Mwaka (1958) na(1962)
Akabeba kama Kocha Akiwa na Brazil Mwaka (1970)
2. FRANZ ANTON BECKENBAUER🇩🇪
Huyu Alikua Mchezaji Raia wa Ujerumani Ila kipindi hicho inaitwa Ujerumani Magharibi (West German.
Aliiongoza Ujerumani Magharibi kama Nahodha(Captain) kutwaa Kombe la Dunia Mwaka (1974).
Na Mwaka (1990) akaiongoza Ujeruman Magharibi hiohio Kutwaa Taji hilo ila mda huu akiwa Kama Kocha.
3:DIDIER CLAUDE DESCHAMPS🇫🇷
Jamaa flani kama Mpole ila very genius na soka na hilo kalidhibitisha kabisa. Huyu ni Raia wa Ufaransa na ndie Kocha Wa Timu ya Taifa Ya Ufaransa kwa sasa.
Huyu ndie anaekamilisha ule UTATU MTAKATIFU wetu.
Enzi za Uchezaji wake alikua anacheza nafasi ya Kiungo Mkabaji.
Amefanikiwa kutwaa Taji hili kubwa akiwa Mchezaji Mnamo Mwaka (1998) akiwa tena kama Nahodha(Captain) wa Timu ya Taifa wakiwafunga Brazil kwenye Fainali Magoli matatu(3). Akaja akalitwaa Tena Hili kombe Mwaka (2018) mda huu akiwa kama Kocha.
Na Sasa amefanikiwa kufika Fainali Mara mbili Mfululizo tena akivunja Mwiko ambao ulikuepo kwa Takribani zaid ya Miaka 50 zaid kua Bingwa Hajawahi fika Fainali Back to back.
Je, Jumapili hii ataweka record nyingine ya kushinda back to back kama Kocha yuleyule? Ni tusuburi na tuone.