Mimi nafikiri haya maswali ya namna hii yangekuwa labda yanatenga nyakati ambazo wamecheza . Maana tutajikuta kila mtu anamsemea mcheza wa kizazi chake yaani ambaye amemshudia . Vinginevyo tutakuwa hatuwatendei haki baadhi ya wachezaji ambao hatukubahatika kuwaona . Kila kizazi au enzi inakuwa na wachezaji bora kwa kila timu . Sasa swali la mtoa mada ili lijibike vyema na kuwatendea wachezaji wote haki ni lazima uanzie nyakati ambazo Simba ilianzishwa mnamo 1936 na wote tulioko humu hatukuwa tumefikirika kuwepo .