Wachimbaji watakiwa kutumia NSSF

Wachimbaji watakiwa kutumia NSSF

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Mwanza.Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele amewataka wachimbaji wadogo kutumia vizuri fursa iliyotolewa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kukopa mitaji ili kununua mitambo kuhakikisha wanamiliki uchumi wa nchi.
Akifungua kikao cha majadiliano kati ya NSSF na Shirikisho la Wachimbaji wadogo Tanzania (Femata) jijini Mwanza jana, Masele alisema lengo la Serikali ni kutumia maarifa kuhakikisha wachimbaji hao wanapata mikopo ya bei nafuu.
“Kikubwa hakuna fedha za bure, fursa mnayopata muitumie vizuri tusingependa shirika hili lifilisike… Serikali haina uwezo wa kuwakopesha wachimbaji wote, lakini maarifa tunayo mnaona tunavyofanya,” alisema.
Masele alisema Sh2.5 bilioni zilizotengwa na Serikali kusaidia wachimbaji hao hazitoshi na kwamba, baada ya mpango mkakati kukamilika anaamini watapata mkopo wenye riba nafuu kutoka NSSF. Naibu waziri huyo alisema iwapo mkakati huo utafanikiwa, anaamini nchi za Afrika zitakuja nchini kujifunza, huku akiwataka kubadilika kuondoka na mawazo mgando.
“Nasikitika sana wachimbaji wa Nyamugusu tuliandaa mpango na GGM (Geita Gold Mine) wanapewa vifaa, wanachimbiwa dhahabu, inasafishwa na inaenda kuuzwa zinaondolewa gharama zote halafu unapewa fedha yako unakula kuku kwa mrija, wamekataa tumeupeleka Rwamugasa,” alisema.
Akimkaribisha Masele, Meneja Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magoro alisema wanapanga mpangokazi ambayo utasaidia kuelekeza jinsi ya kufanya kazi na Femata, hasa suala la mikopo.
“Hakuna atakayeingia NSSF akajuta, tumedhamiria kufanya kazi na wachimbaji waodogo kwa sababu matarajio ya Femata na yetu yanafanana,” alisema Magori.
Awali, Rais wa Femata, John Bina alisema wachimbaji wadogo walikuwa wamesahaulika lakini hivi sasa juhudi za Serikali kuwaunganisha zinaonekana na kwamba, inatumia zaidi ya Sh250 milioni kwa kazi hiyo.



MCL
 
Back
Top Bottom