Wachina 32 walipa faini mil. 591/- kukwepa jela

Wachina 32 walipa faini mil. 591/- kukwepa jela

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Geita imewahukumu raia wa kigeni kutoka China 32 akiwamo Mkurugenzi wa Mgodi wa Eagle Brand Limited kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh. milioni 591.22 kwa makosa manne.

Hata hivyo, washtakiwa hao walilipa faini na kuachiwa huru. Washitakiwa hao (32) akiwemo Mkurugenzi wa Mgodi huo walifikishwa jana Mahakamani hapo majira ya saa nne na dakika 45 asubuhi wakikabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kuwapo nchini kinyume cha sheria, kufanya kazi na kujipatia kipato bila kuwa na kibali, kukwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kampuni kuajiri raia wakigeni wasio na kibali.

Mkuu wa mashtaka wa serikali Mkoani Geita, Bibiaba Kileo, aliambia Mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao walikamatwa kwenye oparesheni iliyofanyika Oktoba 22, mwaka huu katika Mgodi wa Eagle Brand Limited uliopo katika kijiji cha Nyamahuna wakifanya kazi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakma hiyo Bwegoge Obadia, akisoma hukumu hiyo alisema katika kosa la kwanza washtakiwa 31 wamehukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh. milioni 31 kila mmoja Sh. milioni moja, kosa la pili kulipa faini ya Sh. milioni 310 ambapo kila mmoja anatakiwa kulipa milioni kumi.

Katika kosa la tatu ni kulipa Sh.milioni 240 kwa kukwepa kodi ya TRA wakati katika kosa la nne Mkurugenzi wa Kampuni ya Eagle Brand Limited amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni 10 kwa kuwaajiri wageni wasio na kibali.

Mahakama hiyo lililazimika kusimama kwa muda wa dakika kadhaa kutafuta mkalimani wa lugha ya Kichina baada ya wakili wa raia hao wa kigeni, Miyasi Samson Mashauri akisaidiana na Wakili Francis Beatus Kiganga kuiomba Mahakama kuwa na mkalimani wa lugha hiyo kutokana na raia hao kutokuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiswahili, hivyo Mahakama hiyo kutumia Kiingereza na Kichina.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, Wakili Mashauri aliambia Mahakama hiyo kuwa wateja wake wamekiri makosa hayo bila kuisumbua Mahakama na wako tayari kulipa faini hiyo. Walilipa na kuachiwa huru


Chanzo: Nipashe
 
Hongera Rais Magufuli kwa kusimamia Sheria za Nchi. Wachina waligeuza Tanzania shamba la bibi.
 
Back
Top Bottom