Didia
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 719
- 260
Ndg watz wenzangu,
Siku ya leo Nimeenda kkoo kununua mapazia. Katika pitapita yangu nikapita Duka moja la Wachina liko mtaa wa Aggrey. Nikatoa elfu 80 kulipia mapazia. Yule mchina akinifungia mzigo alafu akapotezea Kutoa risiti. Nikadai risiti.
Alichofanya akaniprintia risiti ya 20000. Nikasema mbona risiti ina kiwango pungufu? Akasema hiyohiyo inatosha. Nikamwambia nataka risiti ya elf80. Msaidizi wake ambaye ni mtz mwenzangu akasema kama vp rudisha mzigo wetu tukupe hela yako. Nikajibu mzigo haurudi na risiti mtatoa. Kuona nimewaka mchina akamtuliza kijana wake akaniprintia risiti nyingine ya elf 60.
Nilichokosea nimesoma tu figure ya mwisho bila kuangalia makato. Kwa kuwa ile ya kwanza ilikuwa na VAT nilidhani na hii iko hivyo hivyo Kumbe haijakatwa hata sh. Moja.
Nimeweka risiti hizi mbili ili mlinganishe. Hiyo yenye TIN inayoishia 49 ni Duka la mtz. Ukilinganisha risiti hizi Kuna tofauti kubwa Naomba wataalam wa kodi na EFD watusadie. Risiti ya mchina ni authentic?
Nimesema Wachina Wanakwepa kodi kwa sababu siku za nyuma kidogo nilinunua Vitasa kwenye Duka Lao nikamprintiwa risiti ya elf70 wakati nilikuwa nimetoa zaidi ya laki tatu.
Nilikomaa akaprinti tena.
Kundi lingine linalokwepa kodi ni wahindi na wapemba. Hawa wanajifanya wameorder EFD Bado hawajaletewa hivyo wanakupa risiti ya zamani. Nimekutana na cases hizi Mara mbili.
Mfanyabiashara anapokwepa Kutoa risiti anakwepa VAT lakini pia anakwepa kulipa income tax kwa sababu kiasi halisi cha mauzo yake kwa mwaka hakiwezi kujilikana.
Tufanye kukomboa taifa kutoka kwenye ufisadi huu?
UPDATE LEO TRH4 DECEMBER
Nimeenda kkoo na kukunua mabegi 6 kwa bei ya sh. 48000. Mchina kama Kawa kaprinti risiti ya 24000. Nikamwambia nataka risiti kamili akaniambia niongeze elf 3000 vinginevyo hatoi risiti nyingine. Nikasema elf 3 ya nini na Wewe umetaja beg ni elf 8 kwa bei ya Jumla kwa piece kuanzia piece 6?. Tukabishana sana akatoa hela Nikasema sipokei hela na ninataka mzigo na risiti kamili. Jamaa kagoma kabisa Nikasema ninakushitaki na nimerekodi maongezi kwenye simu. Akaja mchina mwingine akasema mpe risiti.
Tulipoanza kubishana mchina alijifanya hajui kiswahili, yaani Eti haelewi NENO kodi wala VAT.
SERIKARI ISAIDIE TRA JAMANI KIANZISHWE KITENGO CHA USALAMA WAJIFANYE WANUNUZI ILI WAONE MBINU HII CHAFU NA KUCHUKUA HATUA. This is more than serious yaani Wachina wanafanya wizi bila woga.
Kwa kuwa Rais anaonesha ana Nia ya kukusanya kodi Wtz tuamke tusiadie nchi yetu. TRA na USALAMA WA TAIFA WACHUKUE HATUA KTK HILI. Usalam wa taifa usiwe ni kulinda viongozi tu
Nimetaka kuweka risiti hapa nimeshindwa nitaipost mods wailete hapa