Wachina Kariakoo wanakwepa kodi sijapata kuona

Didia

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
719
Reaction score
260
Ndg watz wenzangu,

Siku ya leo Nimeenda kkoo kununua mapazia. Katika pitapita yangu nikapita Duka moja la Wachina liko mtaa wa Aggrey. Nikatoa elfu 80 kulipia mapazia. Yule mchina akinifungia mzigo alafu akapotezea Kutoa risiti. Nikadai risiti.

Alichofanya akaniprintia risiti ya 20000. Nikasema mbona risiti ina kiwango pungufu? Akasema hiyohiyo inatosha. Nikamwambia nataka risiti ya elf80. Msaidizi wake ambaye ni mtz mwenzangu akasema kama vp rudisha mzigo wetu tukupe hela yako. Nikajibu mzigo haurudi na risiti mtatoa. Kuona nimewaka mchina akamtuliza kijana wake akaniprintia risiti nyingine ya elf 60.

Nilichokosea nimesoma tu figure ya mwisho bila kuangalia makato. Kwa kuwa ile ya kwanza ilikuwa na VAT nilidhani na hii iko hivyo hivyo Kumbe haijakatwa hata sh. Moja.

Nimeweka risiti hizi mbili ili mlinganishe. Hiyo yenye TIN inayoishia 49 ni Duka la mtz. Ukilinganisha risiti hizi Kuna tofauti kubwa Naomba wataalam wa kodi na EFD watusadie. Risiti ya mchina ni authentic?

Nimesema Wachina Wanakwepa kodi kwa sababu siku za nyuma kidogo nilinunua Vitasa kwenye Duka Lao nikamprintiwa risiti ya elf70 wakati nilikuwa nimetoa zaidi ya laki tatu.

Nilikomaa akaprinti tena.


Kundi lingine linalokwepa kodi ni wahindi na wapemba. Hawa wanajifanya wameorder EFD Bado hawajaletewa hivyo wanakupa risiti ya zamani. Nimekutana na cases hizi Mara mbili.

Mfanyabiashara anapokwepa Kutoa risiti anakwepa VAT lakini pia anakwepa kulipa income tax kwa sababu kiasi halisi cha mauzo yake kwa mwaka hakiwezi kujilikana.

Tufanye kukomboa taifa kutoka kwenye ufisadi huu?

UPDATE LEO TRH4 DECEMBER

Nimeenda kkoo na kukunua mabegi 6 kwa bei ya sh. 48000. Mchina kama Kawa kaprinti risiti ya 24000. Nikamwambia nataka risiti kamili akaniambia niongeze elf 3000 vinginevyo hatoi risiti nyingine. Nikasema elf 3 ya nini na Wewe umetaja beg ni elf 8 kwa bei ya Jumla kwa piece kuanzia piece 6?. Tukabishana sana akatoa hela Nikasema sipokei hela na ninataka mzigo na risiti kamili. Jamaa kagoma kabisa Nikasema ninakushitaki na nimerekodi maongezi kwenye simu. Akaja mchina mwingine akasema mpe risiti.

Tulipoanza kubishana mchina alijifanya hajui kiswahili, yaani Eti haelewi NENO kodi wala VAT.

SERIKARI ISAIDIE TRA JAMANI KIANZISHWE KITENGO CHA USALAMA WAJIFANYE WANUNUZI ILI WAONE MBINU HII CHAFU NA KUCHUKUA HATUA. This is more than serious yaani Wachina wanafanya wizi bila woga.

Kwa kuwa Rais anaonesha ana Nia ya kukusanya kodi Wtz tuamke tusiadie nchi yetu. TRA na USALAMA WA TAIFA WACHUKUE HATUA KTK HILI. Usalam wa taifa usiwe ni kulinda viongozi tu

Nimetaka kuweka risiti hapa nimeshindwa nitaipost mods wailete hapa
 

Attachments

  • 1448979370475.jpg
    57 KB · Views: 1,562
Hata mie nagombanaga sana na wahindi hasa wa mitaa yagerezan na swahili wananiboa sana,
 
Utaskia ss hatujogop mbona kikwete ni rafiki yetu ona picha alipiga na mume wangu mmmmm ni shidaaaaa
 
T.R.A wanatakiwa watande kila kona kuhakikisha kodi inalipwa vyema
 
Hizi risit mbona zinatofautiana hata layout. Inawezekana huyu mchina anatoa risit fake
 
Nadhani yunahitaji kampeni ya kufa mtu Itakayo husisha vyama vyote vya siasa,.wanahabari na wasanii. Dai risiti uwe ndio wimbo wa taifa. Pamoja na Hayo ianzishwe mifumo ya usalama wa taifa ya kubaini wafanyabiashara wenye tabia hizo. Mtu ajifanye mteja anunue huku akirekodi ushahidi
Mfanyabiashara atakaye pokea pesa huku akijsubiri akumbushwe Kutoa risiti adakwe na kushughulikiwa.

Kampeini ni muhimu Sana ili kujenga uelewa miongoni mwa Wananchi na hususani uzito wa swala hili. Backup ya dola ni muhimu kujenga utisho na baadae mazoea ya Kutoa risiti bila kushinikizwa
 
hawa ni wahujumu uchumi wanatakiwa inatakiwa sheria wakikwepa kodi waende ndani sawa sawa na miezi waliokwepa wakitoka wafukuzwe nchini ndio heshima itakuepo magufuli fanya kazi ajiri vijana wengi wa kufuatilia haya mambo
 
EFD nyingi kwa sasa zimechezewa, na kuna nyingine aziconect na TRA zina print magumashi ipohaja huu mradi ukafanyiwa marekebisho na kuwekewa mtandao wa stock n.k
 
inabidi kuwe na adhabu kali kwa mfanyabiashara asiyetoa risiti. wataanza kutubembeleza watupe risiti.
 
Serikali pia inapaswa kushusha bei ya EFD ili wafanyabiashara wasiwe na sababu ya kupinga kuzitumia. Hili ni swala la msingi. Kama mchakato wa zabuni ktk upatikanaji wake uligubikwa na rushwa au ukiukwaji wa sheria, uchunguzi ufanyike na wahusika wawajibishwe.

Kwa miaka mingi CCM haikutaka Wananchi wajue kuwa wanalipa kodi kila wanaponunua bidhaa. Swala la kuhamasisha ulipaji kodi limeachwa kwa TRA tena ktk msisitizo mdogo. Tunahitaji mapinduzi katika hili.
Watanzania waambiwe kwamba kwa kila sh. 100 inayotolewa kununua bidhaa au huduma Kuna sh. 18 ni hela ya kulipia hosptiali, kujenga barabara, kuleta maji nk. Watu wajue kuwa maendeleo ni Mali Yao. Hiii misemo ya CCM imejenga barabara huku Wananchi wakifichwa Khs uhusika wao na Ujenzi huo zipungue na hata zikome.
 
nafikiri dawa nyingine ni kutonunua kwa watu ambao wanakwepa kodi.zamani watu waliona sawa tu mana kodi zilikuwa hazisaidii nchi lakini kwa sasa hapana,ni tutahujumu uchumi wetu na kumrudisha nyuma magufuli.
 

mkuu hzo mashine ni ghari sana zingeshushwa walau hata 100,000 kwa bei ya 800,000 ni nyingi sana kuimudu kwa siye wenye vimtaji uchwara
 
Risiti zenyewe kampuni tofauti. Moja VAT registered nyingine haina registration. Peleka TRA washughulikiwe waache wizi
 
T.R.A wanatakiwa watande kila kona kuhakikisha kodi inalipwa vyema
Nadhani watu tukijua umuhimu wa kulipa kodi, tutaisaidia vizuri serikali kukusanya mapato. Bila shaka Magufuli atafanya watu wapende kulipa kodi.
 
Wachina ni shiiida! Wanakwepa sana kodi kikweli!

Maduka yote wanayouza viatu vya jumla hali ni hiyo!

No days, wao ndiyo huingiza mzigo mkubwa wa viatu Tanzania, hivyo watanzania hununua kwa jumla kutoka kwenye maduka yao. Ukienda dukani kwao ukachagua sampo unazozitaka, unalipia wao wanakupa karatasi iliyo andikwa kichina, au pamoja na risiti ya tofauti na hela ulizotoa....kisha unaenda stoo kwao kuchukua katoni za viatu ulizonunua!

Ukifika stoo, abazo huwa ni mbali kutoka kwenye frem zao, wanakuambia uwape hiyo risiti ya magumashi na ule ujumbe ulioandikwa kichina! Muda huo, wewe upo nje ya mlango wa stoo zao....na unakabidhi kwa mlinzi, au mchina anyefungua kidirisha kidgo tu.....baada ya muda kidgo mizigo yako inaletwa, lakini huna risiti wala mama yake risiti!

Ukianza kuwa unaleta fyokofyoko za kuulizia risiti, kesho huuziwi tena mzigo, na usipo uziwa means hufanyi biashara. Kwahiyo hali hiyo, inawafanywa wanfanya biashra kuwa wanyonge katika hilo bila ya kuchukua hatua yeyote!

Maduka yenyewe yapo mtaa (si ukumbuki jina), ila anzia kituo cha police msimbazi kama unaenda mtaa wa uhuru, inafuata Fuel Station, then huo mtaa kushoto! Ila siyo hapo tu, hata oppsite ya huo mtaa upande ule mwingine maduka ya viatu na yeboyebo yapo mengi sana ya wachina hasa kwa kazi hiyo!
 

Suala la kudai risit ni zuri lkn lilivyotengenezwa, lilitengenezwa kitapel. Hakuna mfanya biashara atakaye andika bei halisi ya pesa uliyotoa.

TRA hawakuainisha hiyo 18% ya mauzo ilipwe vipi na wapi, na iwapo kila muuzaji akisema atozwe 18% ya bidhaa uliyonunua tayari kodi inayokusanywa inakula faida yake yote na inaingia hadi kwenye mtaji.

kukwepa hasara hiyo ndo hapo kitu cha 200,000/- wanakuandikia risti ya 20,000/- ili ikichukuliwa 18% ya tra, ichukuliwe kwenye hiyo bei mpya isiyo halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…