Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,472
Hebu naomba kuuliza kwa wale walio jikoni kama wamo humu JF, hivi kweli hili suala la Wachina kujenga bandari kubwa bagamoyo, ni kitu cha kweli au ni ahadi za hewani tu? Nimeuliza hivi kwasababu Julius Nyerere Airport waliahidi kuwa watajenga airport, wakachora mchoro mzuri wa tanzanite, wakazungusha hadi ukuta wa mabanzi, matokeo yake naona hata mabanzi wameyatoa na mchoro umebadilika.
Walikikosa kitu gani pale Julius Nyerere wakaamua kuachana na Tanzania wasiendelee kujenga? Pili, hicho kilichowafanya waiache airport hakiwezi kuwafanya waachane na bandari hiyo wanayotutia moyo?
Mimi sitaamini kama kutakuwa na Bandari hadi nione imeshaanza kujengwa, kwa maneno tu hivi najua tunapigwa changa la macho. Kama ni kweli wanaanza kujenga ni lini? Kuna dalili zozote kwa wale walioko serikalini na wale wa Bagamoyo kuwa wameshaanza au wataanza hivi karibuni?
Pili, kitu gani kinatushinda Watanzania kuboresha reli ya TAZARA na reli ya Kati? Kama wamiliki wa malori ndio kikwazo, kweli wametushinda? Kitu gani pia kitatushinda kuunganisha reli ya kati na reli ya TAZARA kuanza kuwa na treni za umeme? Ili mimi nisafiri toka Kigoma hadi Dar es Salaam kwa masaa walau kumi au kumi na mbili kuliko kutembea siku moja, ili container likipakiwa Dar es Salaam lifike siku hiyohiyo mpakani na Burundi na Congo.
Kitu gani kinatushinda Watanzania kubadilisha reli ya TAZARA kutumia umeme kuliko mafuta, si Muhongo anasema 2015 tutakuwa na umeme wa kuuza hadi nje? Sasa, kama umeme tutakuwa nao bwerere, kitu gani kitatushinda sisi kuwa na treni za mwendo kasi na zinazotumia umeme?
Kama vipi hao wamiliki wa malori wanaokwambisha treni waundikwe kikosi kazi maalumu cha kuwadhibiti kwani hao ni wahujumu uchumi na maadui wa maendeleo ya Tanzania. Tanzania tutalala hadi lini jamani? Rasilimali tunazo, tunashindwa kuzitumia kweli?