Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Mbu ni Aduwı mkubwa wa bınadamu.
KWA UFUPI
- Wasema nchini kwao, ugonjwa huo sasa umekuwa historia.
Dar es Salaam. Serikali ya China imetoa msaada wa dawa za malaria zenye thamani ya Sh2 bilioni, katika jitihadaza kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa huo nchini.
Inaelezwa kuwa dawa hizo za Artemisinin, zimetengenezwa nchini humo na zina uwezo wa kutibu malaria kwa haraka kuliko Kwinini.
Makubaliano ya kuipatia Tanzania dawa hizo, yalitiwa saini jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa China Lu Youging wakati Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi.
Katika hotuba yake, Dk Mwinyi alisema kasi ya ugonjwa wa malaria nchini imeshuka kutoka asilimia 18 hadi 10 na kwamba hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya utafiti uliofanywa mwaka jana. "Tanzania kama zilizvyo nchini nyingine, bado tunaendelea kupambana na ugonjwa wa malaria ili kufikia lengo namba sita katika malengo ya milenia,"alisema Dk Mwinyi.
Alisema pamoja na msaada huo wa dawa, China pia imekuwa ikiisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaleta wataalamu wa afya 2,000. Hali kadhalika kufundisha wataalamu na kusaidia ujenzi wa Kitengo cha Moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa upande wake, Balozi wa China Lu Youging, alisema kuanzia mwaka 2006 hadi 2012 nchi yake ilitoa msaada wa dozi 400,000 za dawa za malaria kwa Tanzania. Alisema miaka 30 iliyopita nchi yake ilikuwa inakabiliwugonjwa wa malaria na kwamba sasa ugonjwa huo umekuwa historia. Balozi huyo alisema hali hiyo imetokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuhamasisha watu kwenda hospitali na kupuliza dawa za mbu.
Daktari bingwa wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Edward Tigelea, alisema dawa hizo ni bora zaidi kuliko Kwinini.
"Hii ni kwa sababu tiba yake ni ya kutumia sindano tu tofauti na Kwinini ambayo huhitaji vitu vingi," alisema.
Tanzania imekuwa ikiendesha kampeni mbalimbali za kupambana na ugonjwa wa malaria ambao tishio la afya za wananchi.
Wachina waisaidia Tanzania vita ya malaria - Kitaifa - mwananchi.co.tz