Wachina waliokamatwa na mabilioni Dar ni tone tuu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Kwanza nawahurumia Sana.. Maana hata kama watatoa maelezo ya kueleweka na kupangua kesi. Kiasi watakachorudishiwa ni maumivu

Niwapongeze pia wote watakaoshiriki kwenye hiyo kesi.. Ni wakati wa mavuno mazuri
Wana sheria

Watakaopata tenda ya chakula

Watakaowasaidia huko mahabusu wapate huduma nzuri za msingi na za lazima
Watakaokubali kuwadhamini kama dhamana ikiwa wazi

"Watakaomaliza kesi"
WakalimaniπŸ˜€πŸ˜ŽπŸ’ͺ🏿✌🏿

Hii ni kati ya zile kesi tamu.. Kama ni nyama ni minofu tupu.. Maini parcee.. Wazee wakubwa kwa wadogo wanajipanga ili wawe sehemu ya hiyo fungate

Ndugu zao wavimba macho watajitenga nao mazima.. Kama kuna kitu mvimba macho hakipendi na anakiogopa Sana basi ni police! Hivyo kuhusishwa kwa namna yoyote ile na mtuhumiwa kwao ni nuksi kubwa
By the way hawa waliokamatwa leo tayari habari zao zimeshafika kwenye jumuiya zao.. So asilimia 95 wako busy kuficha mabilioni yao!

Wachina ni wezi na wapiga dili nambari moja duniani. Na wakifika kwenye mataifa legelege yenye sheria barubaru na batubatu huko ndio hufanya kufuru

Hawa benki hutumika kufanya miamala iliyoshindikana kulipwa ama kulipa tasilimu... Hawapendi mambo ya benki wanakwambia ni sawa na nyumba yenye vioo clear!
Na cash yoyote ikiingia bank itatolewa ndani ya muda mfupi

Kuna biashara kubwa Sana ya miamala taslimu inafanywa na hii kabila na kuikosesha serikali mabilioni ya kodi..
Wanakopesha kwa riba
Wanabadilishana dola kwa viwqngo vyao

Wachina wengi wenye hotel na migahawa na supermarkets biashara yao kubwa ni dili za pesa!
Kukopeshana

Kubadilisha pesa za kigeni
Kulipana kupitia "Wechat pay"

Wengi kazi yao ni kutuma na kupokea pesa toka nchi za nje kupitia Wechat pay ambayo haina control ya serikali

Kwa mfano mchina anayekuja kununua ardhi ajenge kiwanda.. Atakuja na pesa kidogo tuu.. Pesa atakayotumia kununua ardhi atapewa hapahapa bongo na wenzake walioko kwenye hiyo biashara.. Naye atawalipa kupitia Wechat pay!
Hiyo biashara itaendelea kwenye manunuzi yote makubwa mpaka kiwanda kinakamilika

Atakapoanza uzalishaji kila shekeli zikijaa atawapelekea walewale ambao watamsaidia kuzituma China kupitia Wechat pay.. Ambapo kinachofanyika ni miamala kufanyika China na pesa ya huku kubaki hukuhuku.. Hapo wanakwepa gharama za serikali na kodi za kufanya miamala ya kimataifa

Majumba mengi ya kichina hapa Dar na kwenye miji mingine mikuu ni micro finance zisizo na vibali! Kumkuta mchina ana bilion 10 ndani ya nyumba ni kitu cha kawaida kabisa kwao!

Kama kesi ya leo sio mchongo bali ni operation.. Uzalendo ukizingatiwa wanaweza kukamata hata trillionπŸ˜‚

Lakini kama wazalendo wenyewe ni hawa wa OPEN SANDARUSI... πŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏ
Your browser is not able to display this video.
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imethibitisha kuwakamata raia wawili wa China, Yao Licong na Wangu Weisi ambao ni wakazi wa Oysterbay Phonex Apartments Kinondoni Dar es Salaam wakiwa na zaidi ya Tsh bilioni mbili ambapo wawili hao walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya ukwepaji kodi na utakatishaji fedha.

Taarifa ya leo Januari 06, 2026 iliyotolewa na TAKUKURU imeeleza kuwa ukamataji huo umefanyika Januari 05, 2026 ambapo wawili hao walikamatwa wakiwa na fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani 707,075 sawa na Shilingi 1,732,333,750. pamoja na Shilingi za Kitanzania 281,450,000 zikiwa ndani ya gari katika mifuko ya Sandarusi.

Fedha hizo zinashukiwa kuwa ni mazalia ya fedha zilizotakatishwa kupitia taarifa za kadi za benki zilizoibiwa kutoka kwa watu mbalimbali nje ya nchi. Watuhumwa hao wameshindwa kuthibitisha uhalali wa upatikanaji wa fedha hizo kwani hawana kampuni au biashara halali zilizowapatia kiasi tajwa na hawana uthibitisho (stakabadhi) wa namna walivyonunua fedha za kigeni walizokutwa nazo.

TAKUKURU imebainisha kwamba ukamataji huo ulishuhudiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay iliyopo katika Kata ya Msasani, Wilaya ya Kinondoni ambaye alithibitisha kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na kiasi hicho huku ikisisitiza kwamba maofisa wa TAKUKURU ndiyo waliomwita Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ili ashuhudie tukio hilo kwa mujibu wa sheria na taratibu za ushahidi na upekuzi (Criminal Procedure Act)

Aidha TAKUKURU imeeleza kuwa Mtuhumiwa Yao Lovong pia alikuwa akitafutwa na TAKUKURU kwa tuhuma za ufunguaji wa makampuni hewa matano (5) yanayochunguzwa kwa makosa ya ukwepaji kodi na utakatishaji fedha kiasi cha Shilingi Trilioni 1.8 ambazo zinadaiwa hazijatozwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019 hadi 2025.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…