Tarehe 28 Juni huko Yuxi mkoani Yunnan China watu waliingia katika Jumba la Makumbusho la Urithi wa Asili wa Visukuku la Chengjiang ili kuchunguza asili ya maisha na kujionea mwujiza na mvuto wa viumbe wa kale.
Jumba la Makumbusho la Urithi wa Asili wa Visukuku la Chengjiang linahifadhi zaidi ya sampuli 60,000 za visukuku vya viumbe wa kale na wanyama hai wa sasa kutoka kote duniani.