Wachumi jitokezeni mmalize utata kati ya Mwigulu na Mpina

Wachumi jitokezeni mmalize utata kati ya Mwigulu na Mpina

juma30

Senior Member
Joined
Jun 25, 2022
Posts
159
Reaction score
459
Wachumi wakubwa Tanzania na mlioko nje ya Tanzania tusaidieni kufanya uchambuzi kati ya Mpina na Mwigulu nani yuko sahihi kwenye hoja ya Mfumko wa Bei na usimamizi hafifu wa Sera za Fedha.

Hebu tuwasikilize kwa makini hawa viongozi wetu wawili alafu mtusaidie uelewa tanzania ni yetu sote.





 
Mwigulu kakasirika ".....hiii ni field yangu na ijua vizuri......." cha ajabu hajajibu hoja hata moja.Ila mawaziri wa awamu hii ni wakali Mwezi wa kwanza alipanwa kuhusu mgao na bwawa akadai wanamuonea, Nape nae kwa ukali akawa anaya tetetea mamkampuni ya simu kuhusu bando. Waziri wa kilimo kabisa yeye nae ana uchochoro wa "......Vita ya Ukraine na Russia.......kovid......ukame...."

Yaani hawachukui hata mda kutafakari maswali wanayo ulizwa bungeni, wanabaki kutia huruma au kuwa wakali. Mbona Mkenda kuhusu matokea jamaa alijibu vizuri kabisa,mimi mwenye kuna vitu nikavipata kupitia yy.
 
Mpina anaweza kujibiwa na Dr Mkuya wa Zanzibar

Mwigullu yuko kisiasa zaidi
 
Huyo Mpina ana hasira ya kuukosa Uwaziri achana nae mkuu
na wewe unakuwa kama mwigulu anaulizwa bilioni 350 kulipwa nje ya bajeti anajibu mambo ya madarasa... na wewe unarudi kule kule hapa watu wanajadili hoja mpina ni mbunge mwakilishi wa wananchi hayo mambo yako ya sijui alikuwa waziri yanakujaje?
 
Mwigulu ni mchumi wa daraja A kabisa wasomi hawana wasiwasi naye!
 
Kama akili ndio hii tunasafari ndefu sana kama taifa kujikomboa kifikra
 
Back
Top Bottom