Wachumi Mlioko Humu Mtusaidie Kufafanua

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Kupitia kutafutatafuta maarifa ili kuwa wa kisasa (up-to-date) kulingana na matakwa ya dunia hii ya mabadiliko (dynamic world), nimekutana na jambo la kiuchumi ambalo sijaelewa tafsiri yake kitaalam na ambalo ninaomba kueleweshwa na weledi wa tasnia ya uchumi. Ni hivi:

1. Uchumi wa China (moja ya chumi kubwa duniani) unakuwa kwa 5.1%

2. Uchumi mkubwa wa Afrika ambao ni Nigeria unakuwa kwa 3.3%

3. Uchumi wa Znz unakuwa kwa 7.1%

4. Uchumi wa Tz (Bara) unakuwa kwa 6% alipouacha Magufuli.

Utata ninaopata ni huu:-

Je, ina maana Znz na Tz (Bara) zinafanya vizuri kiuchumi kuliko Uchina na Nigeria?

Msaada tafadhali.
 
Asilimia wanazitoa kutokana na pato la nchi husika.... Pato la China ni kubwa asilimia 5 tu ya pato lao inaweza kuwa ndio pato lote (100%) la Tanzania ..

Ukuaji wanapima kwa pato la nchi lote ukijumlisha shughuli zote za kiuchumi .
 
mimi sio mchumi lakin ninavyoelewa ni
mfano mapato ya China ni 10B 2022 na 2023 wamepata 10.5b maana yake wamekuwa kwa 5%

Tanzania 2022 mapato ni 1M na 2023 mapato ni 1.5m means tumekuwa in 50%

hii formula inatumika pia kwenye biashara ku rate ukuaji wa kampuni
 
Mfano rahisi chukulia watu wawili wana mishara
Mr A shilling 1000 kwa mwezi
Mr B shillingi 2000 kwa mwezi
Baada ya mwisho wa mwaka wamepata nyongeza
Mr A kapata 10% ambayo sawa na ziada ya sh 100
Mr B kapata 7% ambayo ni sawa na ziada ya Sh 140

Hapa utaona kuwa A kapata nyongeza kubwa ki % lakini B kapata nyongeza kubwa ki fedha sababu alikua na mshahara mkubwa

Sent from my BLA-L29 using JamiiForums mobile app
 
Hapana.
Maana yake bado ni changa kwenye ukuwaji kiuchumi.
 
Mhhh uchumi unakuwa kwa asilimia 50% 😁😁

Yaan 1million to 1.5milion ni ongezeko la 50%

Namimi nipeleke iki chuo nikapate TRAB and TRAT zangu😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…