BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Verdiana Tilumanywa amesema pamoja na umuhimu wa misaada, si jambo la kufurahia kuipokea, kwani aghalabu mtoaji hutarajia mrejesho chanya.
“Anayekusaidia mara nyingi anatarajia kuzalisha kikubwa zaidi ya alichokupa, hatupaswi kufurahia misaada, inatulemaza kwa kiasi fulani. Kwa wingi wa rasilimali tulizonazo tunapaswa kuzitumia kuzalisha cha kwetu,” alisema.
Alisisitiza umuhimu wa kudhibiti upotevu wa fedha zinazokusanywa kutokana na rasilimali zilizopo, badala ya kuzifuja kisha kuendelea kusaidiwa.
Wakati China ikitangaza kuipunguzia Tanzania sehemu ya deni lake la Sh31.4 bilioni, wachumi nchini wamesema hali hiyo itaipa unafuu nchi kuitumia fedha hiyo katika shughuli nyingine za kusisimua uchumi.
Juzi, Tanzania na China zilisaini mikataba 15 ya kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji, miongoni ulikuwepo wa taifa hilo kuipunguzia Tanzania sehemu ya deni hilo.
Mbali na mkataba huo, ulisainiwa wa usafirishaji wa zao la parachichi kutoka Tanzania kwenda China, hatua iliyowaibua wakulima waliosema ni fursa kwa upande mmoja, lakini wanatatizwa na namna ya kuifikia.
MWANANCHI