Ndoa ziwe za wenye mimba au la..ni ishu ya wahusika na Mungu wao.Hao wanaoshangaa kitendo hicho, ina maana wao wako na haki asilimia 100? Utakuta wao ndio wa kwanza kuzini na kushiriki utoaji mimba mradi waonekane kwa nje kuwa hawana dhambi kwa vile matumbo yako flat!
ACHENI HIZO....MNA DHAMBI KUBWA ZAIDI YA KUPATA MIMBA NA KUFUNGA NDOA!
Mkuu B, nimekuwa sambamba na wewe tangu awali lakini hii post yako hapa imenipa kizunguzungu. Ckujua msimamo wako ndo hivyo.Tatizo ni kwamba the whole enterprise is a fraudulent monopoly. The bigger problem here is the fact that god does not exist and therefore the bible cannot be the word of god, and from there everything based on the bible as "the word of god" is confusingly incosinstent and naturally it falls short of godlike wisdom.Huku tunaambiwa anayezini apigwe mawe, kule tunaambiwa asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe, kitabu hicho hicho.
Hili naona sasa limekuwa ni ukosefu wa adabu ama maadili katika jamii..jamani zamani mimi nijuavyo ni mafuruku kufungisha ndoa zikiwa na mimba ndani yake...nakumbuka kuna siku mchunganji mmoja wa lutherano mwaka jana alikataa kufungisha ndoa ya mtoto wa aliekuwa askofu mkuu mmoja moshi uko akisema kama mtaniruhusu kubariki nitabariki ndoa yenu lakini hivi mkiwa na mimba sifungishi ndoa...hakika kuliwaka moto lakini jambo ambalo sikuamini ile ndoa ilichelewa na akaja mchungaji mmoja akafungish na yeye akiwa anaona aibu akaamua kupasua adharani kama si heshima ya askofu babako kwa kweli tuingefungisha hii ndoa
sasa hivi jambo hili limekuwa ni aibu kila makanisa sasa yamekuwa yakifungisha ndoa zikiwa na mimba ndani yake....majuzi nilihudhuria harusi moja pale st joseph kati ya harusi tano tatu wanawake walikuwa wamevimba matumbo yao kama wako theartre wanasubiri kupasuliwa ilikuwa jambo la aibu sana lakini hatimae ilifungishwa huku mapadre wakipiga makelel ya kutorudia tena watu wengine...bado najiuliza hawa watu huwa wanahonga ndoa kufungishwa hivi ama wanawafanya upofu hawa watumishi wa MUNGU....nafikiri makanisa yanaitaji kuwa mstari wa mbele kukemea na kutaa hali hizi.....wazazi imefika wakati wa kuheshimu ndoa takatifu msiwaruhusu vijana zenu kujazana matumbo na kuwatia aibu mbele ya madhabahu....imagine majana nimeenda shuguli moja nikakuta jamaa anaonyesha zile picha za mwanamke za zamani he gafla anamwonyesha yule mwanamke akiwa na bwanaharusi mtarajiwa wamekumbatiana wanalishana sasa nkajiuliza kama mmeshamaliza kila kitu tumeiwa kufanaynini???/
Kazi kwenu mnaotarajia kuoa kuna starehe ukiwa na mtoto ndani ya ndoa...
ARE OUR CHURCHES IS REAL CHURCHES OR JUST A SOCIAL CLUBS?? ARE THEY REAL FOLLOWING WHATS WRITTEN IN THE BIBLE?
Lets go to the basics??
mmh ... nimeipenda hii!
Mheshimiwa!, Nina mtazamo tofauti na "The head of Thread" yako hapo juu.
Nijuavyo mimi, Padre/Mapadre kwa upande wa imani yangu hawafungishi NdOA.
NDOA, inafungishwa au kufungwa na wahusika wenyewe.i.e David na Betty, ila sasa Mapadre/padre anakuwa amesimama kama shahidi wa kanisa na jamhuri/Serikali.
Lakini kuna vimimba vingine havionekani 1-4 month mchungaji atajuaje huyu ni mjamzito ..hii dhambi itakuwa ya wahusika na si mchungaji
labda ile ambayo akitoka kanisani anafikia leba
Umeipenda hiyo kiingereza au hiyo point?
Vimimba au vijimimba? Lol! Mi naona poa tu kuliko kuja kufunga ndoa na mitoto inashuhudia, kama nilivyofanya mimi.