msukule mzembe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2022
- 253
- 302
Juzi jumapili nikasema ngoja niende kanisani kwanza japo nikashiriki na watu katika ibada ya hapa na pale nikachukua kagari kangu ka ist kabovu nikatoka magetoni kipati mbagala hadi keko kanisa la universal.
Ile kutimba ndani kanisanu muhuni sina hili wala lile nikatafuta siti nzuri ya mbele ili nikakae, nikaona pembeni kuna pisi moja imetulia nikaona sio mbaya nikienda kukaa karibu nayo angalau tubadilishane hata chaji mbili tatu, nikaifata nikaisalimia kwa jina la bwana nae akaitikia nikamwambia nampenda nae mlokole yule akajibu ananipenda pia kwa jina la yesu, nikaona leo kitaumana.
Muda wa mchungaji kuja kuhubiri ulipofika nikashangaa kila alipokua akihubiri akiongelea dhambi ya aina yoyote ile ananiangalia mimi na kidole anakionesha kwangu kimtindo mtindo, nikavumilia ila baada ya muda had watu wakaanza kusanuka wakawa wananiangalia, akisema uzinzi basi ataniangalia mimi, ulevi, uasherati na dhambi zote kwangu........................[emoji41][emoji41][emoji41]
Kiufupi wachungaji habari hizo muache, mnatuharibia sana waumini wenu mnatuchoresha kimtindo
Nawasilisha madini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]