Ndugu zangu kuna jambo linanitatiza kidogo, nimemuona mkuu wa Kaya over the week end mitaa ya mlimani city ambako pamoja na mambo mengine naambiwa kulikuwa na show ya wanamuziki fulani wa kutoka nje ya Kaya, na kwa taarifa nilizozipata jana sasa yuko Italia!!
Lakini sijasikia kama alipita pale Same kuwapa pole ndugu zetu waliokumbwa na msiba mzito!!
Wadau mtanisahihisha if I'm wrong!!
JK alionekana kule kwa Msoga baada ya watu wa kijiji ambapo ni asili yake kukumbwa na maafa ya nyumba zao kuezuliwa mapaa baada mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha nyumba nyingi haswa zile za mbavu za mbwa kuanguka... kesho yake akapaa Italia...
hivi JK ni mbunge au rais? Maana kwa records zangu hakuna aliyefariki Bagamoyo lakini Same tumewapoteza zaidi ya Watanzania 20. Anyway mimi c wa usalama wa Taifa huenda wao wanaweza kutupa jibu zuri zaidi ktk hili lakini common senses zetu wengi zinashindwa kumuelewa kabisa huyu baba wa Bagamoyo. Vitu ambavyo siku zote tunajuwa ni priorities kwake ni completely sio priorities na vile ambavyo ni upuuzi wa kutupwa kwake ndio priorities.
Kaya ilipeleka misaada, iwapo angeenda gharama ingekuwa kubwa.
Anaweza kuwa alijisikia kizunguzungu alipotaka kwenda Same. Akashauriwa apumzike. Nimesikia akitoka Roma atakuwa pale uwanja mpya kupokea kombe la dunia (hata sijui tumeshinda lini kombe hili!).
Atakuwa na akina AY, Nameless, Babra Hassan, Gerald Hando,......