Wadau kwa Milioni 17 naweza kujenga apartment 4?

MIL17 NI DOLA AU?
ha ha ha, mkuu anataka kujenga vibanda 4, kila kibanda kwa 4.2m. Naona nondo haweki, choo hakuna, bati jeupe, mbao pori... mlango wa bati.
 
Kuna design inaitwa STUDIO yaani BWALO inaweza sana kujenga hata 8 kwa 17m
 
Wadau naomben ushauri kwa 17mil naweza kujenga apartment nne zenye room moja ya kulala na sitting room plus choo na jiko?

Msaada tafadhali
Kwa hiyo mil.17 unakuta ni pesa ndefu Sana au ? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚..

Hiyo itaishia kwenye kajumba 1 ka vyumba 2 tuu na pengine isitoshe.
 
17m?

Watu mnachukulia simple ujenzi eeh, labda Banda kama haya ya uswahilini hayana hata msingi

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Hawa ndio walikuwa wanashangaa eti camp establishment kutumia mil.7 wakati uko break down bado inakuwa camp ya kichoko..

Utasikia wamepiga,ndio dizaini ya mtoa mada..

Wakati kiuhalisia nyumba ya vyumba 3 Ili iwe imekamilika kwa nafuu zaidi inakula mil.35 na zaidi,kwa pesa yake hiyo pesa itaishia kwa kajumba 1 ka vyumba 2 ..
 
Labda ajenge na kuezeka tuu ,hapo atapata vijengo 2 ila kama haezeki atapata vijengo 4
 
Ndio nimemjibu kwa apartment nne hapana. Labda tatu kwa kutoweka mbwembwe au mbili zenye mbwembwe
Hivi jamani wenzetu mnajenga humi humu Tanzania au mnajenga mbinguni?. Maana haya mahesabu.....duh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…