Wadau LHRC waanza kuichambua Rasimu ya Katiba

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Bi%20Kijo(2).jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikaliyakiongozwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yameanza kuchambua rasimu ya katiba ili kupata maoni ya pamoja watakayowasilisha kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Zoezi hilo la siku mbili kwa wadau hao, lilianza jana jijini Dar es Salaam na wanachama wa mashirika hayo kutoka mikoa 28 hapa nchini walishiriki.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Hellen Kijo-Bisimba, alisema washiriki watafanya kazi ya kupitia na kujadili vipengele mbalimbali vya rasimu hiyo ya mwaka 2013.
Alitaja maeneo watakayojikita kuyachambua katika rasimu kabla ya kupata maoni ya pamojaya kuwasilisha Tume hiyo, ni pamoja na yale yanayohusu haki za binadamu.
Dk. Bisimba alisema wanachama wanaoshiriki kuchambua vipengele hivyo wamegawanywa katika makundi manane, ambao watakutana kwa siku mbili makao makuu ya LHRC ili kuhakikisha wanapata maoni ya kuwasilisha kama wanaharakati.
“Tunataka kuona kama maoni tuliyoyatoa kipindi kile cha kutoa maoni yetu yaliingizwa kwenye rasimu iliyotangazwa na Jaji mstaafu Warioba,” alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
Bi%20Kijo(2).jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikaliyakiongozwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yameanza kuchambua rasimu ya katiba ili kupata maoni ya pamoja watakayowasilisha kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Zoezi hilo la siku mbili kwa wadau hao, lilianza jana jijini Dar es Salaam na wanachama wa mashirika hayo kutoka mikoa 28 hapa nchini walishiriki.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Hellen Kijo-Bisimba, alisema washiriki watafanya kazi ya kupitia na kujadili vipengele mbalimbali vya rasimu hiyo ya mwaka 2013.
Alitaja maeneo watakayojikita kuyachambua katika rasimu kabla ya kupata maoni ya pamojaya kuwasilisha Tume hiyo, ni pamoja na yale yanayohusu haki za binadamu.
Dk. Bisimba alisema wanachama wanaoshiriki kuchambua vipengele hivyo wamegawanywa katika makundi manane, ambao watakutana kwa siku mbili makao makuu ya LHRC ili kuhakikisha wanapata maoni ya kuwasilisha kama wanaharakati.
"Tunataka kuona kama maoni tuliyoyatoa kipindi kile cha kutoa maoni yetu yaliingizwa kwenye rasimu iliyotangazwa na Jaji mstaafu Warioba," alisema.

CHANZO: NIPASHE

GUD move dr.Hellen , we trust you.
 
Back
Top Bottom