Lakini Shamhuna, ambaye pia ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ), alisema Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bali kinachotakiwa ni kujenga utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi ya kushinda na kushindwa.
Mh!!! Ngida1. Nafikiri una point hapo ya kueleza. Hebu fafanua . Unajua sisi wengine si watu wa Zenj, lakini tuna shauku ya kuyajua yale ya ndani ya huko.Nd. Masatu,
Tafadhali zihurumie mbavu zetu!!!
Hayo aliyoyasema Shamhuna ndio msimamo wa SMZ na yale ya Karume ilikuwa babaisha ***** tu! Kwa kweli inatia uchungu, Maalim Seif baada ya miaka zaidi ya 10 ndio sasa anajua maslahi ya Wa-zanzibari? Sasa zogo lote lile lilikuwa la nini? Kwa mimi Seif ndio awe wa mwanzo kupandishwa mahakamani kwa kuwarejesha nyuma Wa-zanzibari kwa ugomvi ambao kumbe sio wa kweli.
-Shamhuna anaongea nadharia tu kama vile Mhadhiri anayetaka kuwababaisha wanafunzi wake tena wale Undergraduates walio katika mwaka wao wa kwanza.Uzuri wa Shamhuna huwa ni mkweli na haumi maneno! Karume anapodai kuwa suala la serikali ya mseto anawaachia Wazanzibari wenyewe ni kuuma maneno bila kuelezea ukweli wa mambo! Seif na Libumba mmeliwa mchana kweupeee!
Shamhuna kamaliza kazi. Hivi Seif kwanini ameogopa uchaguzi mapema hivyo?? Nadhani alijua tiyari kisha shindwa wacha aombe vyeo vya bure.
.......Kwa hiyo usishangae Karume akakubali kuiachia CUF washinde uraisi mwakani japo ccm hawatapendezwa na hilo.
Huogopi nyani wekundu?Hilo halitotokea na kama likitokea basi wengine tutaingia tena JOZANI!!!!