Kusema ukweli mimi ninadoubt kama wengi wetu kwa kipindi kile tunakuwaga tunaelewa hata maana ya kupenda. Mtu anifuate mie kwa umri huo wa chini ya miaka 18 aniambie nakupenda nataka nikuoe ukimaliza shule. Nitamkubalia kama nimevutiwa naye kwa umbole la nje ila pia kichwani mwangu kutakuwa kumejaa ......mashelashela, nimepigiwa vigelegele na pengine zawadi na jinsi nitakavyokuwa malaika au malkia siku ile ya arus- Na wala sitoelewa akitokea mtu atakayenambia Mwj1, jua ukijaolewa itakubidi uvumilie, utakumbana na a,be,che na mafundo mengine ya hali halisi ya ndoani sidhani kama ningemwelewa.
So mimi ni vema wakati wa umri wa aina hii watu wawe marafiki tu mpaka wakijafika chuo na kujiona wamekomaa ndio watamkiane wanataka kuoana. Wavulana waache kuwekeza( zawadi za kawaida, sijui barua yenye manukato, zile kadi zenye wahindi waliokaa kwenye maua) sawa tuma lakini usijiwekezee ukiwa na matumaini ya huko mbeleni. Waache kubaka akili zao ambazo kwa wakati huo bado hazijakomaa.
Eh hapa nimeandika utafikiri Head Mistress anahutubia loh.....unoko tu umenishika! Nisameheni.