Wadau mwenye ufahamu huu ni ugonjwa gani kwa watoto wangu?

Atclkwanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2015
Posts
823
Reaction score
998
Juzi jumapili mtoto wangu wa kiume miaka 12 akawa analalamika kichwa kinamuuma upande mmoja tu kushoto kama amegongwa na kitu, kwa kweli hali yake ilikuwa mbaya mpaka macho yakawa mekundu na sura kumuiva ila baada ya masaa mawili akawa poa.

Jana jumatatu saa nne usiku binti yangu tena miaka 9 hali iliyompata kaka yake ikamtokea ila it was worse alikuwa hataki kulala eneo moja la kichwa kushoto panagonga,basi usiku mzima hatujalala muda wote analia asubuhi kumekucha anaoneka yupo nafuu kalala fofo, na hii inaweza kuwa kwa sababu hakulala usiku akiamka nataka niwapeleke hospital, JF tuna madaktari mbalimbali waliobobea, ,kutokana na maelezo haya , Je wanaweza wakawa wanasumbuliwa na nini.
 
Maamuzi yako ya kuwapeleka hospitali ni sahihi kabisa maana huko watafanyiwa vipimo vyote sahihi, kwa maoni yangu inaweza kuwa malaria
 
Waulize kama wanapata shida ya macho pia..yani kuona maluwe luwe au giza,kizunguzungu kabla ya vichwa vyao kuuma!!itakua migraine headaches
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…