Mwaka juzi nililima mahindi kijijini (mimi nakaa mjini, nimeajiriwa).
Kule kijijini, kuna mama mmoja alikuwa ananisaidia kulisimamia shamba hilo kuanzia kulimwa, kupanda hadi mavuno). Na alifanya hivyo bila mimi kuwepo (kulima kwa simu)[emoji3]. Mimi kazi yangu ilikuwa ni kutuma pesa tu.
Alipovuna, aliniambia kuwa nimepata magunia 150 ya mahindi. Nikamshukuru snaa na nikamwambia, achukue magunia 20 na mimi aniachie magunia 130.
Sasa kuna kipindi nikawa na shida ya pesa. Nikamwambia ayauze mahindi yangu na anitumie pesa. Huu ni mwaka wa pili sasa ananisumbua. Ananiambia anatuma na hatumi. Nawaza kumfuata kijijini, ila nahofia tunaweza kuumizana na mambo yakawa ndivyo sivyo.
Sasa nataka kumfungulia mashtaka. Nataka kumfungulia kesi ya madai.
Taratibu za ufunguaji wa kesi za madai ni upi?
NB:-
Nina ushahidi wa meseji ambazo tumekuwa tunawasiliana nae tangu hatua za mwanzo kabisa hadi sasa.
Nina ushahidi wa meseji za kutuma pesa kwake na meseji za kunijibu kuwa kapokea
Nina ushahidi wa mawasiliano yangu na mtoto/kijana wake ambaye ndiye anafahamu mapatano kati yangu na mama yake.
Nina ushahidi wa sauti/sound clips ambazo nimekuwa nikimrekodi kila nikiongea nae.
Naombeni taratibu za kufuata ili nimfungulie kesi..pia naomba kujua gharama za kufungua kesi ya madai
Na je, naweza kumfungulia kesi ya madai na ya jinai katika kipindi kimoja?