Wadau naombeni msaada wa dawa ya kuzuia kutapika

Wadau naombeni msaada wa dawa ya kuzuia kutapika

The hammer

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
2,397
Reaction score
1,786
Habari kwa wote na pia poleni kwa kazi za ujenzi wa taifa...

Kuna jirani yangu ni wiki ya pili sasa anapata taabu ya kusumbuliwa na tatizo la kutapika..Ilianza kama Malaria na akapewa na mseto pamoja na phenegan kwa ajili ya kutapika.Cha kushangaza amepona malaria ila tatizo ni kichefuchefu na kuatapika mda wote,usiku halali...karudi hospitali na wamemuongezea phenegan hizohizo kawaeleza hizo dawa hazimsaidii lakini ameambiwa yeye si doctor.

Ni dada amepimwa mara 2 hana mimba, naombeni kama. Kuna wadau wanaojua dawa za hospitali au za kienyeji kwa ajili ya kumsaidia huyu dada anasumbuka...ikiwezekana kama mtu anaweza akanitajia vyanzo vya tatizo lenyewe...wakati mwingine hospitali zetu si msaada sana japo kwasababu ya kuzidiwa na wagonjwa.


Asanteni.
 
kutapika ni kiashiaria kuwa mitambo haijakaa sawasawa. Atafute sababu kwa nini anaenselea kutapika. Ametumia dawa za minyoo? Angeweza kutumia broad spectrum yoyote (anaulizia pharmacy tu watamuuzia). Baada ya hapo aangalie kama bado anatapika abadili daktari.
 
Unataka kutibu malaria kwa panadol? Mpeleke hospitali ili mjue chanzo.
 
Amepima ukimwi? Hii yawezekana ni sepsis. Tumia metoclopramide tabs 10mg tds, asitumie zaidi ya siku tano.
 
nikushauri uende hospitali ya juu zaidi kama unaona tatizo lako halijatatuliwa na daktari wa awali.
Kutapika ni dalili ya tatizo na sio tatizo.
 
Amepima ukimwi? Hii yawezekana ni sepsis. Tumia metoclopramide tabs 10mg tds, asitumie zaidi ya siku tano.

ohhhhh my dear Barca much as una nia njema ya kumsaidia huyu mdada lakini sikubaliani kabisa na approach yako ya ku-prescribe ili kutibu dalili na siyo ugonjwa au tatizo lenyewe.

Msaada wako might turn very harmful kwani mdau anaweza kuchelewa ku-consult hospitali/madaktari ili kubaini source ya tatizo then ikam-cost.

Namshauri mhusika aende kwa daktari au hospital, kama hajapona arudi tena au abadili hosptali/daktari
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom