Wadau naombeni ushauri jinsi ya kuwekeza hizi shs. 10,000,000

JERRY

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
630
Reaction score
502
Mimi ni mfanyakazi serikalini hivi karibuni nimekopa shs.10,000,000[miioni kumi] nimegundua wenzangu wengi huwa wanakopa na aidha kununua magari,kununua viwanja au kufanya mambo yasiyo ya kuzalisha mali then makato ya benki yanapoanza majority wanakuwa katika hali ngumu sana, mimi nisingependa hayo yanitokee hivyo naombeni ushauri wenu wadau wa uchumi niwekeze ktk nini haswa kwa mazingira ya sasa kibiashara.

Kwa kuanzia wazo nililo nalo mimi na ambalo bado nalifanyia kazi ni kufungua biashara ya spea za magari na haswa haya madogo tunayotembelea. Ingawa location imekuwa changamoto

nawasilisha
 
Mkuu umechukua mkopo kabla ya wazo au wazo lako ndy lilikuwa hilojilo la spare?
spare zinalipa ukijua spare za kununua na sehem ya kununua.
 
Wazo nililokuwa nalo ni
spare za magari, ingawa location bado ni changamoto
 
Spea zinalipa mkuu,,location unatafuta tuu,,haswa sehem zilizo karibu na gereji nyingi nyingi
 
Mkuu umechukua mkopo kabla ya wazo au wazo lako ndy lilikuwa hilojilo la spare?
spare zinalipa ukijua spare za kununua na sehem ya kununua.

Kama unataka investment ya uhakika baada ya miaka mitatu uvune mara tatu yake.Nilinunua shamba la ekari 2 Kimbjiji, mbali sana kutoka kigamboni mwaka juzi mwezi wa nane kwa chini ya shilingi Ml 2, leo ninataka kuliuza kwa bei ya mil10(maongezi yapo), na shamba hili halina mazao, ila liko karibu na barabara.Ukitokea ukalipanda miti michache sasa a nina uhakika baada ya miaka mitatu unaweza ukaliuza kwa mil 60 na zaidi, ukumbuke shamba liko Dar es salaam,na itakuwa sehemu hot sana muda si mrefu, ukizingatia kwamba daraja la kigamboni linajengwa, na kiwanda kipya cha sementi.Pia kuna maji mazuri yasiyo na chumvi kina kifupi kama utachimba kisima.Ni mahali panapofaa sana.Na pia si mbali na barabara kuu. Mimi nina mashamba kadhaa huko.Ninaliuza mojawapo ili nijenge mabanda ya mifigo shamba lingine kubwa hukohuko.Na mimi nilikopa pia, na sikujua nifanye bisahara gani na mtu mmoja alinishauri kununua maeneo makubwa mpaka sasa namwona kama ni mkombozi wangu.Hii inaondoa hatari(risk) kwa waanzao biashara mpya.Mkopo unanoga kama tayari una wazo bora la bishara tangu zamani, na umeshapima na kukokotoa faida na hasara,na pia mkopo ni mzuri sana kwa wale ambao wana biashara na wanataka kuongeza mtaji ili kupanua biashara.Unaeza kuniandikia ujumbe/kunipigia kwenye 0657011122 ili tubadilishane mawazo.Kwa biahara ya vipuri(spare), unahitaji mtaji wa uhakika kidogo kufuatana na aina ya biashara, pia ujue vizuri mambo ya magari na aina ya vipuri etc.
 
Duuh! Umechukua mkopo kabla hujabuni wazo!
I wish km ningekuwa na asset yoyote ya juu, tungeandikishiana uniazme 2m nijitupe porini huko. Then 60% returns from your money after 1 year. Anyweiii...
 
Spea zinalipa mkuu,,location unatafuta tuu,,haswa sehem zilizo karibu na gereji nyingi nyingi

Kwa mtaji wa 10M unaweza kuanza vizuri hii biashara? imean mtaji wa spears, kumlipa muuzaji,kulipia kibanda kwa mwaka etc. Hebu mtujuze wenye idea ya hii biashara please!
 
wewe mwenyewe upo katika hali mbaya sana. plz fanya hima uwaone business consultants
 

Ndugu yangu kwanza kabisa hoongera kwa mkopo pili ni kosa kubwa sana kuchukua mkopo wakati hujui ufanye nini vishawishi ni vingi mno leo hii utarudi nyumbani mama atakwambia oo hebu wacha tupunguze laki moja tununue vyombo...kwa sababu haukuwa na plan basi utatoa mwisho wa siku utajikuta umebaki na milioni 2 mwisho wa siku waliokupa mkopo wanaikodolea macho nyumba

Tatu ndugu yangu japo hujaelezea uzoefu wako wako katika masuala ya biashara kwa haraka haraka naona hauna uzoefu wa biashara na kama hauna uzoefu wa biashara basi ni bora ukawa mwangalifu lazima ujue hizi biashara za uchuuzi unahitaji uwe na uzoefu kwanza wa biashara yenyewe pili uzoefu na unachotaka kuuza kuna jamaa mmoja alichukua kinua mgongo chake chote basi akaamua kukitupa kwenye biashara ya samaki ..kaenda mwanza kachukua mzigo aliporudi dar samaki wote wameoza mwisho wa siku akaanza kuwatafuna mwenyewe na majirani...namaanisha nini?Biashara ya spea pia zinahitaji ufaahamu wa spea zenyewe kwa undani moja ukizifahamu ni rahisi sana kuwapata wateja kwa kuwa utakuwa na uwezo wa kuwashauri lakini kama huzifahaamu tabu kwa kuwa wewe mwenyewe kuna siku utauziwa feki

Ushauri wangu:
1)Jaribu kuangalia biashara ambazo ni imovovable kwa mfano ardhi kama mdau mmoja ailivyokwambia-usioende kujiingiza kwenye biashara zinazotegemea mood ya watu-jiingine kwenye biashara zinazotegemea mahitaji ya watu-Siku za nyuma nimewahi kumshauro mdau mmoja hapa -mfano unaweza kukamata mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti ukatengeneza mafuta mwenyewe na kuwauzia wenye magenge-siku ya siku utajikuta biashara inakua kufikia malengo
2)Unaweza kukamata ngome watano wa maziwa nakuwaweka nje ya mji-siku ya siku kila ngone anatoa maziwa lita 30 kwa siku-30x5-150 mfano lita moja shilingi 2000 basi kwa siku una 300000 kwa mwezi 9000000 hayo ni makadirio tu

3)Kama unahisi huwezi kutengengeza faida unayo hitaka basi ni bora ukaingia mkataba na kampuni fulani changa ukaweka pesa ukawaka unakula dividend

Kama utahisi unahitaji ushauri zaidi basi unaweza kuwasiliana na mimi nikakupa ushauri zaidi
 
Mil 10 ni nyingi ukizitamka lakini ukianza kuzifanyia mchakato ni ndogo sana ushauri kama upo maeneo ya tegeta tafuta duka la vifaa vya umeme. Ni biashara ambayo inalipa sana anza na product za nyumbani ukiona mtaji umekuwa jipinde dubei utakuja kunieleza kwa maelezo ukihitaji zaidi ni pm haiana presha na watu wanajenga kila siku wanahitaji hivyo vitu
 

thanx mdau nimekusoma vizuri sana, be blessed
 

Lima matikiti, kwa kila heka unapata faida ya milioni 2 mpaka 3.5. na yanachukua siku 60 mpaka kuvunwa. Mimi nina eneo linalofaa kwa kilimo hicho Kigamboni KM 24 kutoka ferry na panauzwa kwa milioni 1 kwa heka.
 
lima matikiti, kwa kila heka unapata faida ya milioni 2 mpaka 3.5. Na yanachukua siku 60 mpaka kuvunwa. Mimi nina eneo linalofaa kwa kilimo hicho kigamboni km 24 kutoka ferry na panauzwa kwa milioni 1 kwa heka.

eneo linaitwaje, na maji ya kumeagilia je yapo?
 
Kama hujielewi bora ukanuue hisa ukiwa unawaza nini cha kufanyia.

Spare parts zinalipa sana, kuanzia za pikipiki au magari, profit margin yake ni 500%. Ukiweza kuzifuata dubai utakuja kusimulia.
 
Lima matikiti, kwa kila heka unapata faida ya milioni 2 mpaka 3.5. na yanachukua siku 60 mpaka kuvunwa. Mimi nina eneo linalofaa kwa kilimo hicho Kigamboni KM 24 kutoka ferry na panauzwa kwa milioni 1 kwa heka.

heka 1 ya matikiti inakuwa na wastani wa miche mingapi mkuu? kila mche unakuwa na matikiti mangapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…