Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Wadau,
Naamini weekend inaendelea vyemaaa!
Mods tafadhalini huu uzi uacheni hapa hapa msiupeleke jukwaa la michezo, maana huu ni zaidi ya taarifa za kimichezo. Tunaongelea utaifa zaidi hapa.
Anyways, kama mjuavyo wadau, timu yetu ya taifa imefanikiwa kushiriki kwenye michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) itakayofanyika nchini Egypt kuanzia 21st June 2019. Hii itakuwa mara ya pili kwa nchi yetu kushiriki katika michuano hii, na iliposhiriki mara ya kwanza mwaka 1980 wengi wetu tulikuwa hatujazaliwa na waliokuwa wapo duniani tayari hawakuwa na uwezo wa kwenda na timu huko Nigeria kulikofanyika michuano hii kutokana na sababu mbali mbali.
Bahati nzuri mwaka huu na kipindi hichi Watanzania wengi wanaweza kwenda na timu huko Egypt kwa sababu gharama pia sio kubwa kivileee. Kwa hiyo shime watanzania twendeni Egypt tukai-support timu yetu na kuipeperusha bendera yetu.
Michuano ya mwaka huu itafanyika kwenye viwanja sita ambavyo vipo katika miji minee ambayo ni Cairo, Alexandria, Ismailia na Suez. Jana groups zilipangwa na bahati nzuri sisi tumepangwa group C pamoja na Kenya, Algeria na Senegal na Uwanja tuliopangiwa sisi ni Al salaam stadium/ 30 June Stadium ambao upo Cairo. Hii maana yake ni kwamba, Watanzania tutakuwa pale pale Cairo kwa mechi zote za Makundi ambazo tunacheza mechi ya kwanza dhidi ya Senegal mnamo tarehe 23 June saa mbili kamili usiku, mechi ya pili dhidi ya Kenya mnamo tarehe 27 June saa tano usiku na mechi ya mwisho ya makundi dhidi Ajgeria mnamo tarehe 1 July saa nne usiku.
RAI KWA TFF: Kwa vile wengi wetu vipato vyetu sio vikubwa hivyo, tafadhalini harakisheni utaratibu mzima wa sisi mashabiki kuweza kwenda Misri (kama huo mpango mnao) na muutangaze mapema ili tujue gharama na kwa wale waajiriwa waangalie utaratibu wa kuomba ruhusa makazini mwao.
Kama tujuavyo nchi hii wapigaji ni wengi, tafadhalini sana TFF msije mkadhani hii ni fursa ya kutangaza gharama za hali ya juu ili mpate "kupiga", jueni kwamba mashabiki katika mpira wa miguu ni mchezaji namba 12 na timu zetu zinawahitaji mashabiki, hivyo basi gharama ziwe chini kwa kadri iwezekanavyo.
Mimi binafsi kwa vile nimejiandaa kwenda Egypt kui-support timu yetu na taifa letu, nimeamua kufanya research fupi ya gharama za kwenda na kukaa angalau kwa siku kumi (mpaka mechi za makundi zimalizike) na gharama ni kama ifuatavyo.
RETURN FLIGHT TICKET
Departing Dar Es salaam on 19th June
Arriving Cairo on 20th June
Departing Cairo on 2nd July
Arriving Dar on 2nd July
TOTAL PRICE will be USD 470.00 which is equivalent to TZS 1,128,000.00 (rate 2400)
HOTEL FOR 12 NIGHTS
Pyramisa Suites Hotel in Cairo USD 100.00 per night (for two people)
Marvel Stones Hotel (Breakfast included) TZS 100,00/= per night kwa chumba cha watu wawili na kwa chumba cha mpaka watu wanne ni TZS 177,096.25 per night
Panorama Pyramid Inn ni TZS 138,899 per night (Breakfast included) kwa watu wawili.
NB: HOTEL NILIZOANGALIA MIMI NI "FIRST CLASS HOTELS"
Kutakuwa na gharama za visa ambazo ni USD 50
Kutakuwa na gharama za match day tickets ambazo kwa kweli sijui.
Makadirio ni kwamba isimgharimu mtu mmoja zaidi ya 2,500,000/= kwenda kwenye safari hii na kuishi nchini humo kwa muda wa siku 12 comfortably.
Wadau tafadhalini ongezeeni gharama nyengine ambazo nimeziacha either kwa kuzisahau au kutozijua.
Karibuni wale wote ambao tuna nia ya kuelekea kwenye michuano hii na tusubirini utaratibu wa TFF, pengine gharama zitakuwa nafuu zaidi maana tunazo "madege" yetu na gharama zinaweza shuka.
Naombeni kuwasilisha.