Sikushauri kijana mdogo uingie kwenye hiyo mitandao yaki Pyramid.
Ni afadhali mara 10 uniambie unafyungua kigenge hapo kwenu, unaenda tandale/buguruni unaleta mzigo unauza reja reja.
Au unafgungua kibanda cha Chips
naliweka hili jamvini ili nipate kujua,kwa kifupi mimi ni graduate wa level ya bachelor,lakini ajira imenipa kisogo kwa miaka miwili yaani cjawahi kuajiriwa sasa nimeona nijiajiri lakini juzi nilipata bahati ya kuingia kwenye mkutano wa wadau wa gnld nikaelezwa mengi ambayo yamenishawishi kufanya hiyo biashara japo nijikimu kidogo sasa nilikuwa nawauliza wadau hususan wale ambao wamejihusisha na wanajihusisha na hii biashara ,je faida ni kama tunavyoshuhudiwa na watu kwenye mikutano ,kama ndivyo ni namna ipi ya kuifanya biashara hii vizuri? Na zipi ni changa moto zake? Asanteni wadau
ukiishi kwa kusikiliza ya watu utasanda maisha yako yote !!!! Mimi nafanya hiyo biashara part time na napata kipato kizuri cha ziada na sio ngumu kama unavyofikiria !!!! Niko kwenye kampuni tofauti na yako !!!! Nimesoma ninajua faida za kujituma kwa bidii.......sasa kama unaishi kwa maneno ya watu...pole sanaaa !!!!!!!!
mkuu nimekusoma ni pm basi unipe realities za hiyo unayofanya
MKUU KAMA UNAMTAJI WEWE KOMAA NA AIDEA YAKO YA BIASHARA ACHANA NA HAWA WATU, NI SAWA NA FOREVEL LIVING,
- Hawa watu ukienda kwenye mikuatano yao watakueleza mambo matamu sana na watakumbia biashara pekee duniani ni ya kuuza hayo madawa na kutafuta wanachama iko kama UPATU,
- Haya makampuni huwa wanatunga story za mafanikio na wanawawekea mikanda ya watu wanao dai walikuwa masikini sana lakini baada ya kujiunga na mtandao wao wamekuwa matajiri sana
- Huwa hata wanaleta watu waliopikwa waje kuwambia wao walukuwa mafundi viautu na sasa ni matajiri, wengine utaambiwa walikuwa ma hose girl na sasa ni matajiri
- Kwa kifupi kwenye marketing wako vizuri sana wana lugha za kuvutia watu kujiunga nao na wana story nzuri sana
MKUU SASA NJOO KWENYE VITENDO, HAPO NDO UTAGUNDUA NI KWA NINI SIKU ZOTE THEORY NA PRACTICE HUWA ZINAPINGANA
MKUU NI VIGUMU SANA NI LAZIMA UJUE KUDANGANYA WATU NA MADAWA YAO NI GHALI SANA NA INABIDI UZUNGUKE KUTAFUTA MEMBERS SEHEMU MBALIMBALI
MKUU ILA KUJA KUFIKIA WATU ULIONYESHWA MIKANDA YAO KWENYE POWERPOINT SI LEO WALA KESHO INAWEZA KUKUCHUKUA MIAKA 15 HADI 20
Ndio walewale wazee wa desiukiishi kwa kusikiliza ya watu utasanda maisha yako yote !!!! Mimi nafanya hiyo biashara part time na napata kipato kizuri cha ziada na sio ngumu kama unavyofikiria !!!! Niko kwenye kampuni tofauti na yako !!!! Nimesoma ninajua faida za kujituma kwa bidii.......sasa kama unaishi kwa maneno ya watu...pole sanaaa !!!!!!!!