Wadau wa elimu: Contents za mtaala ulioborshwa umezingatia umri?

Nyamesocho

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2023
Posts
487
Reaction score
1,287
Nimewasikia watekelezaji wa mtaala (walimu) na wanafunzi kupitia wazazi wanasema mada zinazofundishwa darasa la tatu zinawadi umri mfano
Kwenye somo la hisabati,jometri iliyokuwa inafundishwa darasa la tano sasa ipo darasa la tatu,Jiografia na mazingira,Sura ya nchi iliyokuwa inafundishwa darasa la sita sasa ipo darasa la tatu, wengine wanadai maudhui ambayo yanafundishwa kidato cha kwanza somo la sayansi(physics,chemestiry na Biology) Sasa wanafundishwa darasa la tatu,siyo hiyo tu mpaka maana ya katiba anaanza kufundishwa darasa la tatu

Je katika kuandaa contents serikali imezingatia umri na uelewa wa mtoto ?
 
Mbona kenya hayo mambo ndo wanafundishwa wakiwa darasa la tatu dunia imebadilika mzee vitu vya darasa la tatu unataka ufundishwe form two
 
Hii inaumiza Sana watoto bado ubongo wao haujakuwa kuweza kubeba vitu vikubwa kichwan mwa Mtoto wa miaka 7,8,9. Hawaelewi chochote ni mzigo Sana kwao. Watoto wengi wa shule za kidumu na mfagio unakuta hata kkk hawajui. Hayo masomo wanayajulia wapi?

Ndo kuua kwenyewe elimu yetu hivyo. Na ndo maana hakuna mtihani wa wa necta wa class seven
 
Mbona kenya hayo mambo ndo wanafundishwa wakiwa darasa la tatu dunia imebadilika mzee vitu vya darasa la tatu unataka ufundishwe form two
Tuna viongozi wajinga Sana Tena Hawa wa ccm. Ni janga la taifa Kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…