Wadau wa elimu tumsaidie dada huyu aliyedhurumiwa cheti chake..

King Kimwe

Senior Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
130
Reaction score
30
Habari za saa hizi wanajamii...
wiki iliyopita nilikua mkoani singida katika harakati zangu za kusaka mkate wa kila siku lakini safari haikuishia singida mjini kwani ilinilazimu kwenda katika wilaya moja wapo ya mkoa huo inaitwa ITIGI...
Hapo nilikutana na dada mmoja akiwa na watoto wawili mmoja anamiaka ka mitano ama minne hv na wapili ni mdg zaid aweza kua na miez nane hv ama mwaka mmoja...
Yule dada alikua mbele yangu nafikiri alikua anakwenda hospital grafla alikutana na wanafunzi ambao walikua wamevalia ngua za manesi bila shaka wanasomea utabibu hapo itigi waliongea kisha wakaachana wakaendelea na safari mimi nikawa nimemfikia yule nlipomuangalia vizuri nikagundua alikua akilia kwa kwikwi..
Nikamsemesha "dada vp mtoto kazidiwa.. Akanijibu hapana, ikabidi nimdadisi ndipo akanisimulia...
Anaitwa TAUSI KHAMIS KASUKA alimaliza elimu ya secondary mwaka 2005 Itigi secondary na kufaulu kwa division four poit 28 lakini kila akijaribu kufatilia cheti chake ili angalau ajiunge na chuo anazunguushwa tu na mkuu wa shule yan dhairi cheti chake kumeuzwa kwa mtu mwingime na kinatumiwa ''ebu fikiria kaka toka 2005 naambiwa cheti bado hakijaletwa na baraza kweli inaingia akilini na kilichoniuma ni kuwaona awa wadogo zangu nliowaacha shule wanasoma unes mi ninawatoto wawili sina mbele wala nyuma jamanni..."
Aya ndungu zangu yoyote mwenye uwezo wa kumsaidia dada apate cheti chake na mkuu kuchukuliwa hatua nita mp no ya dada..
aksanteni
 
daah inauma kweli! Ila sina uwezo wa kumsaidia, ngoja wenye uwezo waje
 
Kwanza pole yake sana na inasikitisha kwa kweli, kunyakuliwa haki yako hasa ambayo umeipigania miaka minne....

Kuna Jamaa mmoja hivi aliwahi kufanyiwa hivohivo alikua akihadithia tukiwa kwenye basi ,alichokifanya alienda kumshtaki mwalimu mkuu mahakamani na ahatimaye likipata cheti chake.
Nenda jukwaa la sheria watasaidia mawazo mazuri.........
 

aksante kaka
 
aende mahakamani kufungua shauri la madai ya cheti chake, ila akumbuke kuwa na result sleep, admission number, living certificate kama ipo. mahakamani watamsaidia tu pia atatakiwa adai fidia kwa uzembe ulifanywa na mkuu wa shule kumkawizia cheti hicho tangu kipindi hicho
 
aende TAKUKURU ALAFU mahakamani kufungua shauri la madai ya cheti chake, ila akumbuke kuwa na result sleep, admission number, living certificate kama ipo. mahakamani watamsaidia tu pia atatakiwa adai fidia kwa uzembe ulifanywa na mkuu wa shule kumkawizia cheti hicho tangu kipindi hicho
 
sawa tumepata,namuonea huruma sana.kama una namba yake ya form 4 NA MAJINA YAKE NIPE NIJARIBU KUPITA NECTA,NA NDO IWE MWANZO WA KUANZA PROCESS ZA KWENDA MAHAKAMANI HATIMAE TAKUKURU,ALIETUMIA CHETI CHAKE ALAANIWE NA ASIENDELEE MPAKA AJISALIMISHE NA ARUDISHE.AMINA
:frusty:
 
aende TAKUKURU au atafute taasisi zinazohusika na maswala ya kisheria atasaidiwa.
 
Aende baraza la mitihani akiwa na ; kitambulisho chochote kama birth certificate, au vote card akiambatanisha na form 4 result slip au index number. Ukweli utajulikana tu.,asikate tamaa.
 
Aende baraza la mitihani akiwa na ; kitambulisho chochote kama birth certificate, au vote card akiambatanisha na form 4 result slip au index number. Ukweli utajulikana tu.,asikate tamaa.

Ushauri mzuri. Tatizo jingine kwa Wahanga kama huyu ni namna ya yeye kulifikia hilo Baraza la Mitihani kwa maana ya gharama za safari na uoga wa Urasimu anaoweza kukutana nao hapo Baraza. Pengine ingekuwa rahisi kama angekuwa na mtu wa "kumshika mkono" hapo Dar na kumsaidia kwenye mchakato wote. Inasikitisha na inatia machungu!
 

Kaka, kwa kuwa JF ni kusaidiana, naomba na mimi nikusaidie kidogo. Sio "result sleep" bali ni "results slip" na sio "living certificate" bali ni "Leaving Certificate" katika misingi ya Mada iliyopo. Tuko pamoja, Kaka!
 
Reactions: keh

kaka nimejaribu kumpigia leo yupo kijiji cha pili kilioni pia akanambia hakumbuk namba yake wala ya shule mpaka atakapo rudi nyumbani kisha ata nitumia si unajua kitambo kidogo toka amalize...
 
kaka nimejaribu kumpigia leo yupo kijiji cha pili kilioni pia akanambia hakumbuk namba yake wala ya shule mpaka atakapo rudi nyumbani kisha ata nitumia si unajua kitambo kidogo toka amalize...
sawa mkuu nimekupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…