Waandaaji wa filamu nyingi za bongo mnaboa sana, hivi hamjajua tu kuwa hadithi za filamu zenu nyingi hazivutii? Unaweza kuwa na kipaji cha kuigiza, halafu usiwe mtunzi mzuri. Kila mtu mungu kampa kipaji chake. Hadithi ndio msingi wa filamu bomba, nchi inao watunzi waziri wa hadithi waliobobea. Mfano Erick Shigongo, Beka Mfaume, Hussein Tuwa, Juma Kidogo, Sultan Tamba na wengineo. Mkiwatumia hawa, mnaweza kujikuta mnatengeneza filamu zenye viwango na ubora wa hali ya juu.
Hivi umefanya utafiti kabla hujaandika uliyoyaandika au umekurupuka tu
ili mradi nawe uonekane unajua kukosoa? Kwanza nakubaliana nawe kuhusu
filamu za Bongo kuboa kwa kuwa kila mtu sasa anadhani kuwa anaweza
kutunga wakati kuna watu waliopewa vipaji vya utunzi. Lakini sikubaliani
kabisa na wewe kuhusu aina ya watunzi uliowataja kwa kuwa nawafahamu
vizuri, Eric Shigongo amekuwepo kwenye game na ametunga hadithi
kadhaa zilizotengenezwa movie (kama Fake Pastors, Froma China With Love)
na hazina tofauti na hizo filamu zingine za Bongo zinazoboa. Sultan Tamba
ndiye kinara wa kutunga hadithi za filamu nyingi ambazo hazina kichwa wala miguu...
Beka Mfaume na Hussein Tuwa ni watunzi wazuri wa riwaya lakini hawana uwezo
wa kuandika script kwani script ina misingi yake na hata hadithi zao zina mambo
ambayo ili kuyafanikisha kwenye filamu zetu unahitaji kuwa na bajeti kubwa mno
ambayo kwa soko la Bongo ni sawa na ndoto za mchana. Juma Kidogo hana tofauti
na baadhi ya watunzi ambao hadi sasa wameshindwa kulipenya soko letu kwa kuwa
ili filamu iwe bora kama unavyosema inapaswa kuwa bora katika mambo matano na
si hadithi peke yake kama unavyotaka watu waamini. Pia ieleweke kuwa mtunzi mzuri
bado hakukusaidii kuifanya filamu iwe nzuri kwa kuwa huijui misingi ya uandishi wa script
(mwongozo andishi wa filamu)...
Filamu nzuri lazima iwe imekamilika katika mambo haya: (i) Script nzuri, (ii) Waigizaji wazuri,
(iii) Muongozaji mzuri, (iv) Wapigapicha wazuri, na (v) Mhariri mzuri. Katika haya utagundua
kuwa ubora wa filamu hautegemei hadithi tu ambayo hata hivyo inapaswa ipate mwandishi
wa script mzuri katika kuijenga (dramatise) na kuisuka (plot) katika namna ya kusisimua,
kuvutia na wakati mwingine kuhuzunisha kutegemeana na kisa chenyewe.