Wadau wa kiswahili

Babaticha

Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
26
Reaction score
1
Napenda mnijuze Maana ya Silabi na Njia zinazotumika katika Uundaji wa Silabi
 
Nijuavyo mimi...... Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za lugha hutamkwa mara moja kama fungu linalojitegemea kimatamshi na fungu hilo linaweza kuwa na sauti moja kulingana na lugha husika hususani muundo wa lugha hiyo.
...... Njia za uundaji wa silabi
(a) K+I mfano ka,ma n.k
(b) K+K+I mfano mku+bwa silabi 2 hapo.
(c) K+K+K+I mfano skru+bu silabi 2 hapo.

(d) K peke yake mfano m+moja m imesimama peke yake na ni silabi inayojitegemea kimatamshi
(e) K+1/2 I mfano bwe+ni .bwe ndio ya muundo huu.
(f) muundo wa K+I+K mfano kab+la kab ndio ya muundo huu
(g) muundo wa irabu peke yake mfano u+a= silabi 2

MUHIMU: k imetumika kuwakilisha konsonanti I irabu na 1/2I nusu Irabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…