Wadau wa Magari, vipi gari aina ya Mitsubish Outlander

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,422
Reaction score
7,350
Wadau wa magari naomba muidadavue Mitsubishi outlander hii SUV body yake na muonekano umenivutia.

Sasa nataka kujua ,udhaifu wake ni UPI katika safari ndefu na pia service zake na ubora wake
 
Mkuu hii mashine mimi binafsi naikubali sana engine yake ni 2.4L kama harrier, nilienda siku moja car wash kuna jamaa alikua nayo akawa anasema alivyoitoa bandarini ilikuja na nusu tank yeye akaijazia full tank akaenda nayo hadi morogoro akaipiga misele na akarudi nayo mafuta bado yalikuwepo registration ya jamaa ni DRJ maana yake haina hata miezi miwili bongo nadunduliza ikifika $3500 naliagiza.

kiukweli haya magari sio mengi nadhani spare zake hazitakua nyingi ila nitanunua hivyo hivyo likizingua spea nitapaki naagiza mbele ikifika naendelea na misele.
 
Ahsante kwa ufafanuzi Jana hapa Dodoma nimemuona kuna MTU amepaki hiyo Mahakama kuu namba D ,ngoja nipambane niagize chuma
 
Wadau wa magari naomba muidadavue Mitsubishi outlander hii SUV body yake na muonekano umenivutia ..

Sasa nataka kujua ,udhaifu wake ni UPI katika safari ndefu na pia service zake ..na ubora wake
Mi ninayo tangu January mwaka huu. Kiukweli ni gari nzuri sana, na nimesafiri nayo, Dar-Arusha-Dar. Dar-Ifakara-Dar, Dar-Mor-Dar, Dar-B/Moyo-Dar na Dar-Dodoma-Dar bila matatizo yoyote. I would recommend one to buy.

Binafsi haijanisumbua hadi sasa, cha kuzingatia ni aina ya oil inayotumia mfano yangu ni 2009 model 2.4L, Engine oil inatumia 5W-20 na Transmission yake ni CVT na inatumia J1-Type so hakikisha unaweka oil sahihi wakati wote, being CVT inasaidia kupunguza fuel consumption kiasi fulani..

All the best mkuu.
 
ilikugharimu kiasi gani mpaka kufika mikononi mwako?
 
Kuna sehemu niliikuta hii gari wanaiita kubwa jinga sijui ni kwanini hata mkuu.
[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]

DAAAAAAAH!!!
HII NCHI INA RAIA WAKOROFI SANA HII!!!
 
From outside imesimama kweli kweli. Hope ni moja ya small SUV zinazovutia. Ngoja niicheki ndinga
 
If you wont mind. How much for the price?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…